Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, August 21, 2015

Tunataka sera za vyama siyo matusi kampeni za uchaguzi.

NA EDITOR

21st August 2015

Katuni.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), imetangaza kesho kuwa ndiyo siku ya kuanza kwa vyama vya siasa kampeni za kuwanadi wagombea wake wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi.
Nafasi zinazowaniwa na wagombea hao ni za udiwani, ubunge na urais.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichoko madarakani katika serikali inayomalizika muda wake, kimemteua Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kupeperusha bendera yake kwa nafasi ya urais.
CCM imejipanga kuzindua kampeni zake Jumapili wiki hii katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Rajabu Luhwavi, alikaririwa juzi na gazeti hili akisema baada ya uzinduzi huo jijini Dar es Salaam, itafanya kampeni zake katika maeneo yote ya nchi na imepanga kufanya mikutano 1,000 sawa na wastani wa mikutamo 15 kwa siku moja.
Aidha, alisema chama hicho kimejipanga kuhakikisha kinawafikishia watu wote ujumbe unaokusudiwa katika takriban siku 63 za kampeni.
Kwa upande wa mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, chama hicho kilipanga kuzindua kampeni zake kesho Jumamosi katika Uwanja wa Taifa.
Hata hivyo, serikali imezuia shughuli za kisiasa kufanyikia katika uwanja huo wa kisasa wenye uwezo wa kubeba watu waliokaa kwenye viti 60,000.
Hivyo, hadi kufikia jana, Ukawa walikuwa hawajatangaza rasmi mahali gani jijini Dar es Salaam watazindulia kampeni zao.
Nipashe linapenda kutoa rai kwa vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi mkuu katika nafasi yoyoye ile ya uongozi, kuhakikisha kwamba kampeni zinafanywa kistaarabu.
Tunatarajia wagombea watajikita zaidi kuelezea ilani za vyama vyao jinsi vilivyojipanga kuwaletea wananchi maendeleo na si kusimama majukwaani na kuporomosha matusi ama vijembe visivyo na tija.
CCM  tayari imetangaza timu yake ya kampeni ilivyosheheni makada 32 wenye sifa za kila aina.
Watanzania wanatarajia kuwasikia makada hao wakimwaga sera za chama chao kiungwana ili kuwashawishi wawapigie kura wagombea wao.
Kama ilivyo kwa CCM, basi pia Watanzania watapenda kusikia sera za kutoka upande wa upinzani zikielezwa kwa lugha ya kistaarabu ili kutoa nafasi kwa wananchi kuzipima na hatimaye ifikapo Oktoba 25, mwaka huu, watumie haki yao ya kikatiba kuwapata viongozi wao kutoka katika vyama hivyo.
Watanzania yatupasa kufahamu kwamba amani iliyopo ikitoweka, ni kazi kubwa kuirejesha.
Ni kwa msingi huo ndipo tunapowasihi wagombea wa vyama vyote kuacha kufanya kampeni za kukamiana na kutumia lugha za matusi kati ya wagombea wenyewe kwa wenyewe ama vyama kwa vyama.
Nec nayo inapaswa kuhakikisha kwamba inapanga vizuri mikutano ya kampeni pasipo kuingiliana kwa ratiba ama viwanja vya mikutano kwani hali hiyo yaweza kuwa mwanzo wa uvunjifu wa amani.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment