Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha UPDP, Mhe Mwajuma Ali Khamis akiwasili katika viwanja vya ukumbi wa Salama Bwawani tayari kwa kuchukua Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar kupita Chama chake, akiwasili katika Afisi za Tume ya Uchaguzi zilioko katika Ukumbi wa Salama Bwawani.
Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Salum Kassim Ali akitowa maelezo na kumkaribisha Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi kukabidhi Fomu kwa Wagombea wa Urais wa Zanzibar katika Ukumbi wa Salama Bwawani.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jecha Salum Jecha akimsomea Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar Mhe Mwajuma Ali Khamis kabla ya kumkabidhi kushuhudia Wananchi waliomshikikiza kujua yaliomo katika fomu hiyo.
Mgombea Urais kupitia Chama cha United People Democratic Party(UPDP) Mwajuma Ali Khalis akifuatilia kwa makini maelezo yaliokuwa yakisomwac na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar wakati wa hafla ya kuchukua Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar.
Mgombea Urais kupitia Chama cha UPDP Mhe Mwajuma Ali Khamis akionesha Fomu yake ya Kugombea Urais wa Zanzibar baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Mhe Jecha Salum Jecha katika Afisi za Tume Bwawani Ukumbi wa Salama
/ZanziNews.
No comments :
Post a Comment