Mhe Lowassa ambae kaandikiwa barua ya wazi na waliokuwa raia wa Tanzania wanaoishi nje wakimtaka atamke waziwazi kama anaunga mkono uraia pacha.
Barua hio alioneshwa muakilishi wa Zanzibar Ni Kwetu (ZNK) wa nchi hio na ambae hakuruhusiwa kuchukuwa kivuli chake kwasababu Wana-Diaspora hao hawakutaka majina yao au nchi wanayoishi kutangazwa kutokana na sababu za usalama wao, ili anza kwanza kwa kumuamkia Mhe Lowassa.
Barua iliendelea kuwa..." Tumeiona namba ya mjini Dar Es Salaam, ya Mbeya, ya Arusha, ya Mwanza na ya mjini Zanzibar. Tungelifurahi kama nasi tungenafasika kuiengeza hio namba katika ghafla yako yoyote ile ijayo, lakini haitowezekana, kwani tupo mbali na nyumbani".
Wana-Diaspora hao wamelielezea blog la Zanzibar Ni Kwetu kuwa wao sio wanachama au wapenzi wa chama chochote kile hapa nyumbani.
"Chama chetu kinaitwa TANZANIA. Tunaipenda sana nchi yetu ya Tanzania na yoyote anaeitakia mema tunampenda nae pia", alieleza mmoja wa Wana-Diaspora hao wakati muakilishi wa ZNK akiendelea kuisoma hio barua huku wameketi kwenye mkahawa mmoja mdogo kwenye corner ya barabara mbili maarufu za mji huo.
Barua inaendelea kueleza kuwa, ..." Sisi Wana-Diaspora tutawashinikiza ndugu, jamaa, wazee na yoyote yule aliekuwa wetu huko nyumbani kukusindikiza wewe katika safari hii ya matumaini ya nchi yetu, lakini tunataka kwanza utuwekee wazi juu ya mambo haya matatu, kama wananchi wa Tanzania watakuchagua wewe kuwa Rais wa Jamhuri hio October 25, 2015".
Barua hio ya wazi kwa Mhe Lowassa iliendelea kuyaeleza mambo hayo matatu kuwa ni ...
“[1] Kwanza, tunataka mzee Lowassa utuhakikishie kama mtizamo wako juu ya Wana-Diaspora sio ule wa sisi kuonekana kama ni maadui na ni hatari kwa usalama wa nchi yetu, kama wengine wanavyotuona".
“[2] Pili, tunataka mzee Lowassa utuhakikishie kama utatuwezesha Watanzania sote tunaoishi nje ya nchi au Wana-Diaspora wote ambao tunaostahiki kupata uraia pacha tupate, ili tuweze kushiriki kikamilifu katika shughuli tofauti za kuiletea nchi yetu maendeleo ya kweli”.
Item hii iliendelea kwa bold capital letters na maneno kuwekewa mstari chini kuonesha kwamba ni maneno muhimu sana na ikaendelea kueleza kuwa….”TUNACHOKITAKA SISI MHESHIMIWA LOWASSA NI URAIA PACHA NA SIO VITAMBULISHO (I.Ds) KAMA VILE SISI NI REFUGEES. VITAMBULISHO HUPEWA REFUGEES NA SIO WAZAWA AMBAO KWA BAHATI MBAYA MAISHA YAO WANAYAENDESHA KWA HUKU NJE, LAKINI ROHO NA MIRADI YAO YOTE IPO HUKO HUKO NYUMBANI.
MHESHIMIWA LOWASSA, KATIBA ILIYOPENDEKEZWA IMETUDHALILISHA SANA NA IMETUFANYA SISI KAMA TULIKUWA RAIA WA KUJA HUKO TANZANIA".
MHESHIMIWA LOWASSA, KATIBA ILIYOPENDEKEZWA IMETUDHALILISHA SANA NA IMETUFANYA SISI KAMA TULIKUWA RAIA WA KUJA HUKO TANZANIA".
[3] Tatu, tunakuomba Mhe Lowassa kama utachaguliwa na wananchi basi Katiba inayopendekezwa uirejeshe tena kwa mzee Warioba ili aipitie na airekebishe kama vile ilivyokuwa mwanzo - yaani kama vile wananchi aliyowahoji huko nyuma walivyotaka.
Barua hio ya wazi ilimalizia kwa kuandika kuwa, ….”Needless to say, utakapoingia madarakani utakuwa mwenye mengi ya kuyaweka sawa, kwasababu wapo mamilioni ya watoto, ndugu, jamaa na wananchi wenzetu ambao bado wakienda kulala usiku matumbo yao yanapiga manyanga. Sio hilo tu Mheshimiwa, kumbuka kuwa watoto wetu bado mashuleni wanakaa chini kwa wale waliobahatika kupata shule, kwani wengi wanasoma chini ya miembe na mibuyu, huku wakubwa wakihongana bilioni 1.6 kila mmoja. Watoto wetu mashuleni ndio wakushughulikiwa kwanza", ilimalizia barua hio na huku ikimtakia Mhe Lowassa kila la kheri na ushindi wa kishindo tarehe 25 October, 2015.

Wandugu,
ReplyDeleteMmeniwakilisha na mimi pia.
Maneno msumari kwa Lowassa.
Ayafanyie kazi sasa hivi na atutamkie kinaganaga kama anaunga mkono dual citizenship au vipi.!