Wafuasi wa Ukawa katika uzinduzi wa kampeni za umoja huo zilizofanyikan juzi katika Viwanja vya Jangwani.
Vyama hivyo ambavyo vimemsimamisha mgombea mmoja kupitia Chadema, walifanya ufunguzi huo kwa kuzingatia kanuni na maadili yaliyowekwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Katika uzinduzi huo, mgombea urais, Edward Lowassa alipata dakika chache za kuwaeleza wananchi mikakati yake ya kile atakachokitekeleza kwa miaka mitano endapo atapewa ridhaa ya kuwatumikia.
Hata hivyo, Lowassa hakuweza kuisoma hotuba pamoja na Ilani ya uchaguzi ya chama chake na kuwataka wananchi waisome kupitia kwenye tovuti ya chama hicho.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Lupa Ramadhan alisema:
“Hotuba ya kuisikiliza ni tofauti na ile ya kuisoma.
Kuna kitu wafuasi wa Ukawa na Watanzania kwa ujumla walikikosa baada ya mgombea kupatiwa muda mchache wa kuzungumza kwa kuhofia kuvunja sheria. Nina imani waandaji wataliona hilo na watalifanyia kazi ili lisitokee siku nyingine,” alisema Dk Ramadhan.Katika uzinduzi huo, mgombea urais, Edward Lowassa alipata dakika chache za kuwaeleza wananchi mikakati yake ya kile atakachokitekeleza kwa miaka mitano endapo atapewa ridhaa ya kuwatumikia.
Hata hivyo, Lowassa hakuweza kuisoma hotuba pamoja na Ilani ya uchaguzi ya chama chake na kuwataka wananchi waisome kupitia kwenye tovuti ya chama hicho.
Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Lupa Ramadhan alisema:
“Hotuba ya kuisikiliza ni tofauti na ile ya kuisoma.
Mkutano huo ulihamasisha watu wengi kujitokeza kumsikiliza mgombea lakini kiu yao haikukatwa, alisema Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Hamad Salim.
“Wengi walitka kusikiliza hotuba ya mgombea pamoja na kujua ilani na sera ambayo haikukatwa baada ya mgombea kushindwa kumaliza hotuba yake ambayo ndiyo iliyowafanya wamfuatwa,” alisema.
Profesa Andrew Temu wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA), alisema mkutano huo haukutoa tafakuri ya kina ya namna ya kupunguza au kuondoa umaskini licha ya ukweli kuwa uchumi wa nchi unakua kwa kasi nzuri. “Kampeni ni fursa ya wanasiasa kukuna vichwa na kuonyesha jinsi wanavyoweza kuwa wabunifu kwenye Ilani zao kwa kuainisha changamoto na adha za wananchi na namna ya kuzitatua kwa mipango ya uhakika. Hii inatakiwa iende mbali zaidi ya kutoa ahadi.
Makamu Mkuu wa Chuo cha RUCO, Profesa Gaudence Mpangala alisema mkutano huo ulitawaliwa na vijembe kutoka kwa makada wa CCM waliohamia Chadema.
“Nilitarajia suala la katiba mpya lingeongoza ajenda,” alisema.
ya Ilani yao kwasababu umoja wao unatokana na hilo. Mengine waliyoyaahidi yanafanana na wapinzani wao. Hata walioikosoa Ilani ya CCM walibainisha hilo na nilichokitarajia ni kuona wao wanalifanyia kazi ili kujitofautisha nao,” alisema.
/Mwananchi.
No comments :
Post a Comment