Marehemu Mohamed Mtoi enzi za uhai wake ,kushoto ni gari aliyopata nayo ajali.
Mgombea ubunge wa jimbo la Lushoto, mkoani Tanga kwa tiketi ya Chadema, Mohamed Mtoi amefariki baada ya gari lake kupinduka wakati akitokea kwenye kampeni.
Akithibitisha taarifa hizo zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii jana usiku, Katibu wa Chadema wilayani Lushoto, Abdalah Dhahabu amesema ajali hiyo imetokea jana jioni wakati mgombea huyo akitokea Mlola alipokuwa anafanya kampeni kuwania kiti hicho.
“Ni kweli Mtoi ametutoka na hapa nipo nyumbani kwa marehemu Mkunzi. Hapa (jana usiku) tunangojea taarifa za wanandugu tujue taratibu za maziko,” amesema katibu huyo.
Akieleza namna ajali ilivyotokea, Dhahabu amesema wakati Mtoi alipomaliza mkutano wake wa kampeni Mlola, alipanda gari kurudi nyumbani kwake eneo la Mkunzi ndipo lilipoacha njia na kupinduka na mwanasiasa huyo kufariki papo hapo.
Akizungumzia hali ya dereva wake, katibu huyo amesema alikimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Lushoto na kwamba afya yake ilikuwa inaendelea vema.
No comments :
Post a Comment