Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, September 5, 2015

Chifu Yemba, mpinzani wa Lipumba anayewania urais

Mgombea urais kupitia ADC, Chifu Yemba akikabidhiwa nyaraka za uchaguzi Mkuu na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu, Damiani Lubuva.
Baada ya jitihada zake za kumuondoa Profesa Ibrahim Lipumba kwenye uenyekiti wa chama cha CUF, Chifu Lutayosa Yemba sasa ameanza safari mpya ya kuelekea Ikulu, akipeperusha bendera ya Alliance for Democratic Change (ADC).
Chifu Yemba alikuwa mwenyekiti wa CUF wa Wilaya ya Shinyanga na alikuwa amepania kupambana na Profesa Lipumba kwenye mbio za uenyekiti wa chama hicho, ingawa wakati huo hakuonekana kuwa alikuwa akianza safari ya kuelekea Ikulu.
Lakini harakati zake za kushika wadhifa wa juu wa CUF ziligonga mwamba baada ya Baraza Kuu kuchukua uamuzi wa kumtimua kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha na kutumia vibaya jina la mwenyekiti wake.
Akiwa mjumbe wa Baraza Kuu la CUF, Chifu Yemba aliona kuna uwezekano wa kupindua uamuzi huo na hivyo kuandika barua ya rufaa kwa katibu mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad. Hata hivyo, hakuweza kutengua uamuzi huo.
Akizungumza na waandishi wakati huo, Chifu Yemba alisema CUF ilikuwa imepanga kumtimua muda mrefu kutokana na misimamo yake kwenye vikao vya chama.
Alisema ndio maana iliundwa kamati ya kuchunguza taasisi anayoiendesha na zikakusanywa taarifa alizoziita za uongo kupata sababu ya kumfukuza.
“Zilikuwapo kamati tatu zilizonichunguza nasikitika walitoa taarifa za uongo kulilazimisha baraza lichukue uamuzi,” alisema.
“Waliamua kuwarekodi watu kwa maelekezo yao binafsi na kwa makusudi wakatumia maneno hayo kama uthibitisho. Utaratibu walioutumia kunifukuza, sijaridhika nao na nimekataa rufaa kupinga uamuzi wa baraza,” alisema Chifu Yemba.
Kwa mujibu wa Chifu Yemba baada ya uchunguzi huo hakupewa nafasi ya kujitetea wala hakuwahi kusomewa mashtaka badala yake baraza lilimpa hati ya mashtaka nusu saa kabla ya kikao cha kutoa uamuzi.
Safari hii ameibuka upya, akiwa chama hicho cha ADC ambacho kimempa fursa ya kuwania urais.
Yemba anasema iwapo atachaguliwa kuongoza Taifa la Watanzania, mambo manne atayapa kipaumbele; kuboresha huduma za afya ili kila Mtanzania awe na afya bora, huduma za maji, kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi, kutumia rasilimali zilizopo kuboresha maisha ya watu.
Anasema asilimia 78 ya Watanzania hawana afya bora na kwamba kutokana na idadi hiyo kubwa itakuwa vigumu kwa watu wa aina hiyo kujiletea maendeleo.
Anasema kwa kuwa Tanzania ina rasilimali nyingi, atazitumia ili kuboresha huduma za afya ili kila mtu bila kujali ana kipato cha aina gani aweze kupata huduma hizo.
Kuhusu maji, Yemba anasema hicho ni kipaumbele kingine muhimu na anaungana na mgombea mwenzake Rakesh kusema maji yamekuwa yakiwatesa Watanzania kwa muda mrefu
Anasema serikali haijawa na nia ya dhati katika kukabaliana na tatizo la maji ndiyo maana hata bajeti katika miradi ya maji zimekuwa hazitekelezeki.
“Tanzania ina kiu ya maji na utafiti wangu umebaini kwamba asilimia 20 tu ya Watanzania ndiyo wanaopata maji safi na salama baada ya zaidi ya miaka 50 ya uhuru, huu ni utani,” anasema.
Anasema asilimia 74 ya ardhi ya Tanzania ina maji ya kutosha na kwamba kutowapatia wananchi maji safi na salama ni kuwapuuza.
Mgombea huyo anasema akichaguliwa atahakikisha anadhibiti mianya ya ukwepaji kodi hasa kwa kuangalia upya utoaji wa misamaha ya kodi.
“Hatuwezi kupata maendeleo kama tutaendelea kutoa misamaha ya kodi, nitalishughulikia eneo hili kikamilifu ili kuinua maisha ya Watanzania.
Pamoja na kwamba alipania kupambana na Lipumba kuwania kiti cha uenyekiti wa CUF, Chifu Yemba anaonekana hana kinyongo na uamuzi wa Baraza Kuu kumtimua uanachama.
Wakati Profesa Lipumba alipotangaza kujivua uenyekiti wa CUF kwa maelezo kuwa dhamira inamshitaki kutokana na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kumpa fursa kada wa zamani wa CCM, Edward Lowassa kuwania urais, Chifu Yemba alimuomba msomi huyo wa uchumi ajiunge na ADC.
Alisema iwapo Profesa Lipumba angekubali kujiunga na ADC, alikuwa radhi kumuachia agombee urais kwa tiketi ya chama hicho na yeye abaki mwanachama wa kawaida.
“Lipumba amekuwa mvumilivu sana na nampongeza kwa hilo kwa maana alitegemea mabadiliko lakini haikuwa hivyo, hatimaye ametoka. Kama akikubali kujiunga ADC kabla ya saa 5:00 kesho, nitamuachia agombee urais,” alisema Chifu Yemba.
/Mwananchi.

No comments :

Post a Comment