dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, September 7, 2015

Moro gharika JK mshangao.

Rais Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete amekiri hajawahi kuuona umati kama uliojitokeza jana mjini Morogoro wakati mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, alipohutubia kwenye mkutano wake wa kampeni.
 
Akizungumza kabla ya Magufuli kupanda jukwaani, Rais Kikwete alisema katika kipindi chake chote (cha kuwa madarakani), hajawahi kuona watu wengi mjini humo wakifika kwenye mikutano ya CCM kama ilivyokuwa jana.
"Lazima niseme ukweli... sijawahi kuona umati kama huu (mjini Morogoro)," alisema Kikwete.
 
Aidha, alimtaka Magufuli kutokuwa na hofu ya ushindi kwani kwa uungwaji mkono mkubwa anaopata kwa wananchi, ni wazi kwamba atashinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu na kwamba "wanaojiita Ukawa watabaki na ukiwa" baada ya Oktoba 25.
 
Ukawa ni kifupi cha muungano wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ambavyo vimemsimamisha Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa. Vyama hivyo ni NCCR-Mageuzi, NLD, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama cha Wananchi (CUF).Aliyasema hayo jana mjini Morogoro wakati akihutubia mamia ya wananchi waliojitokeza kwenye uwanja wa Jamhuri mjini hapa ikiwa ni mwendelezo wa kampeni za mgombea huyo ambaye leo ataelekea mkoani Tanga.
 
Alisema atakapostaafu mwaka huu na kwenda kupumzika, atakuwa na amani na atalala usingizi mzuri kwa kuwa atakuwa amemwachia nchi mtu mchapakazi na mwadilifu ambaye anawapenda Watanzania.
 
“Tarehe 25 msibabaike, rais anayetosha ni Dk. Magufuli na kwa dalili hii mlivyojitokeza kwa wingi naamini wenzetu Ukawa watakuwa wakiwa baada ya uchaguzi, CCM imefanya uamuzi wa busara kuwaletea Magufuli, hivyo siku ya kupiga kura msifanye makosa,” alisema Kikwete.
 
Alisema  kwenye mchujo wa urais, majina yote yalijadiliwa kwa haki na mwishowe kupata majina matatu yaliyopelekwa Mkutano Mkuu ambapo mgombea Dk. Magufuli aliibuka mshindi kwa kura nyingi, hivyo wanaodai kuwa Lowassa alionewa hawana hoja.
 
“Lowassa asiwadanganye kwamba hakujadiliwa, kwenye Halmashauri Kuu. kulikuwa na mjadala mkali na mrefu sana hadi tukakubaliana kupata kura za kupata majina matatu ambayo yalipelekwa kwenye mkutano mkuu, kule aliyeibuka mshindi ni Dk. Magufuli tena kwa kura 2,000 kati ya 2,400, huu ni ushahidi tosha kwamba mgombea wetu anakubalika,” alisema rais Kikwete.
 
MAKAMBA AMVAA LOWASSA
Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Yusuf Makamba, ambaye alikuwa kivutio kwenye mkutano huo kutokana na namna anavyonukuu vifungu vya Biblia kwa ufasaha, alisema Lowassa alipaswa kuwa jela muda huu na anamshangaa kapata ujasiri wa kugombea urais.
 
Alisema mgombea huyo wa urais kwa tiketi ya Ukawa alishapanga kuihama CCM tangu mwaka 1995 baada ya jina lake kukatwa katika mbio za urais na kuongeza kuwa ana mambo mengi mabaya kuhusu mgombea huyo ambayo Watanzania wengi hawayajui.
 
Makamba alisema jina la Lowassa lilikatwa kwenye mbio za urais CCM mwaka 1995 na yeye (Makamba) alipohoji kwanini jina hilo limekatwa, alijibiwa kuwa huyo kijana yaani (Lowassa) ni mdogo, lakini  ana mali nyingi ambazo ameshindwa kuzitolea maelezo.
 
 “Niliomba aitwe ahojiwe kuhusu mali zake, lakini hayati Baba wa Taifa alikubali kwa sharti kwamba swali hilo nimuulize mimi, alipokuja Lowassa nilimuuliza watu wanahoji wewe ni mdogo sana lakini una utajiri mwingi wanahoji ulipataje pataje, alinijibu kwamba ana mali kama Watanzania wengine,” alisema Makamba.
 
Aidha, alisema Lowassa alipobaini kuwa yeye (Makamba) alimtetea kwenye Nec), alimwandikia barua akihoji kama kuna sababu za yeye kuendelea kukaa kwenye chama hicho katika mazingira ambayo yanaonyesha hawamtaki.
 
Makamba alisema alimshauri Lowassa kutohamia upinzani kwani kwa kufanya hivyo angekuwa sawa na kuruka matope na kukanyaga kinyesi.
 
AMVAA PIA SUMAYE
Kuhusu Sumaye, Makamba alisema Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, ni mvumilivu kwani alikaa na Waziri Mkuu mzigo kwa miaka 10 ambaye kwa wakati huo hakuwa hata na Shahada ya Chuo Kikuu.
 
Alisema Sumaye alikwenda kusoma shahada nje ya nchi baada ya kustaafu ili apate sifa za kuwa rais na kwamba alitumia madaraka yake vibaya katika kipindi chake cha miaka 10 kwa kutwaa ardhi kubwa mkoani Morogoro ambayo bado hajaiendeleza.
 
Naye mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, amewataka Watanzania wamchague kuwa rais ili apambane na hatimaye kuwafyeka mafisadi wachache waliobaki serikalini na pia kudhibiti zaidi wafujaji wa fedha za umma.
 
Kadhalika, amesema mafisadi wachache waliopo ndiyo wanaoiyumbisha nchi na hivyo akichaguliwa, kazi yake ya kwanza itakuwa ni kuwaondoa na kudhibiti matumizi yasiyo ya lazima ili fedha zinazookolewa zisaidie maendeleo. 
 
Magufuli aliyasema hayo jana wakati akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza kumsilikiza kwenye mikutano yake mbalimbali ya kampeni kwenye majimbo ya Kilombero, Mikumi na Kilosa na mjini Morogoro.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment