Wakati Mukoba akiyasema hayo, mgombea Urais Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, ameahidi atakapoingia madarakani, atahakikisha elimu inatolewa bure kuanzia shule za awali hadi chuo kikuu.
Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, kupitia ilani yao wanayoinadi hivi sasa, imeahidi elimu bure kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu.
Katika mahojiano na Nipashe Jumapili, Mukoba alisema elimu bure ilikuwa inawezekana kwa kipindi kirefu lakini tatizo lipo katika mfumo wa uongozi.
Alisema fedha nyingi zimeelekezwa sehemu tofauti huku sekta ya elimu ikibaki kuwa na changamoto.
“Tunapoambiwa elimu bure ninavyoelewa mimi ni kwamba fedha za kuendesha sekta hii na nyingine zitatokana na kodi zetu,” alisema na kuongeza:
Alisema ikiwa mfumo wa ukusanyaji kodi wa sasa utaendelea kama ulivyo, suala la elimu bure halitawezekana.
“Nchi kama Botswana kule wanachimba madini na mwekezaji kwenye sekta hiyo anatoa asilimia 50 serikalini, Ghana wao wamefanikiwa kuwaboreshea walimu mishahara yao, kwa nini sisi tushindwe,” alihoji.
Aliongeza kuwa, walivyokwenda kupanua elimu kimataifa walikubaliana watenge pato la ndani la taifa asilimia sita, lakini Tanzania haijawahi kutenga hata asilimia mbili.
Alimtaka kiongozi ajae atoe kipaumbele cha kwanza katika elimu kwa kuhakikisha changamoto za vitendea kazi, maabara, walimu na upungufu wa madawati vinapatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Naye, Mkuu wa Kitengo cha Sayansi na Siasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana, akitoa maoni yake, alisema suala hilo litawezekana ikiwa litatekelezwa kwa awamu.
Alisema kama walivyoanza na shule za msingi, baadaye wanatakiwa kwenda mbele zaidi kwenye shule za sekondari na kumalizia chuo kikuu.
“Kama watatoa elimu bure na kuibana sekta nyingine kwa kuiongezea malipo ili kufidia, itawekana. Ila wanaoahidi wanatakiwa kufanya uchunguzi wa kutosha kwenye ahadi hii na kuwaeleza Watanzania vyanzo vya mapato vya ziada watavipata wapi,” alisema.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments :
Post a Comment