Hakuna shaka kua ccm wanataka kufanya wizi wa kubadilisha matokeo ya kura za Uraisi,vipi matokeo ya kila kituo yanajulikana baada ya umalizikaji wa kupiga kura katika kituo husika halafu leo uambiwe usitangaze nani kashinda katika kituo na nani kashindwa na kura za uraisi kujulikana ni gapi kwakila kituo ili kuweza kujua yupi kashinda na yupi kashindwa.
Hapa pana shaka kubwa na Serekali ya ccm kufika hadi kuwawekea mkwala wangalizi wa kimataifa kua wasitangaze takuwimu wala kufika katika maeneo mengine wasio ruhusiwa .
Ikiwa vyama vilivyounda Umoja wa UKAWA vitakubali ujanja na Ulahai huu Basi hakikisha jawabu ni fupi tu, watakae mtangaza ni JOHN POMBE MAKUFULI na wakisha maliza kumtangaza hapo ndipo watadilina Wangalizi wa Jumuia za Kimataifa na nchi zao na hakuna shaka jumuia za Kimataifa zita bweka tu hakuna tena litakalo badilisha matokeo.
Kuna tetesi kua siku ya upigaji kura vyombo vyote vya Ulinzi (Dola) wameshaambiwa viongozi wao kua waweze kufanya iwezekanavyo lakini John Makufuli aibuke Mshindi na Ali Mohammed Sheni, Siku ya kupiga kura kutakua na vidisho na vitimbi vyakila aina lakini ikiwa Wananchi watataka kweli Mabadiliko basi uchaguzi wa Mara hii Ulimwengu wote unaitupia Jicho Tanzania kuona hali siku ya Uchaguzi itakuwaje?
Wananchi wa Tanzania wakishindwa kuiondoa ccm madarakani Oktoba 25, Basi wasubiri tena miaka 50.
No comments :
Post a Comment