Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, September 12, 2015

USHUJAA WA LOWASA


Kwa miaka miwili tu ya Uwaziri Mkuu, alifanya makubwa sana zaid ya walikoaa miaka 10, pia aliwaonesha na kuwafundisha KWA VITENDO KAMA IFUATAVYO:

1.UMUHIMU WA ELIMU AWALI, kwa kuanzia ujenzi wa shule za kata ...lakini tangu alipoondoka ukadolola na kuisha.

2.UMUHIMU WA ELIMU YA JUU..kwa kuhimiza na kusimamia ujenzi UDOM kwa nguvu zote ujenzi ukafanyika..alipoondoka, mpaka leo majengo mengi UDOM hayatumiki (wanafunzi wa UDOM watakuwa mashahidi wa hili), ...waliobaki serikalin wameshindwa hata kufadhilia wanachuo wa kutosha !! vijana wapo mitaani kwa kukosa ufadhili...HII AIBU SANA kwa nchi yenye rasilimali kama Tz.

3.UADILIFI WA VITENDO..Pale serikali ilipokumbwa na kashfa ya Richmond, alijiwajibisha kama waziri mkuu,ili kuiokoa serikali...toka alipoondoka kashfa nyingi zimetokea,wizi mwingi umetokea,ufisadi mwingi umetokea, Taarifa ya CAG imeonyesha hata wizara ya MAGUFULI UFISADI UMETOKEA..lakini wameshindwa kuelewa somo la UADILIFU KWA VITENDO alilowaonyesha kwa vitendo, ..wameshindwa kujiwajibisha.!! Sasa wanatudanganya uadilifu kwenye mapango..wahanga wanasema.."chema chajiuza chenyewe..hakihitaji promo"

4. UJASIRI NA UZALEDO, alipoteuliwa Mwkt wa kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama alionyesha msimamo dhabiti na pia hotuba kali kwa Rais wa Msumbiji aliyetaka kuingilia mipaka yetu..Na yule mama akakoma...Lakini wameshindwa kuiga mifano yake..mpaka panya road wanatikisa jiji!!..mpaka vituo vya polisi vinavamiwa na Polisi kuuwawa!!..wamekuwa HAWANA UZALENDO WA KULINDA RAIA, wamekuwa DHAHIFU NA LEGELEGE!!

5. HAKI NA USAWA, aliweza kusadia kufanikisha maji ya ziwa victoria kufika mpaka mikoa ya Shinyanga,Tabora. Hakuweka umimi kushughulikia maji Monduli pekee, Sio kama Magufuli alivyoindisha mpango wa barabara na kulazimisha zipite jimboni kwake Chato..huu ni UBAGUZI !!..Toka ameondoka wameendeleza UBINAFSI na UBAGUZI..Mwingine alilazimisha Nyumba ya speaker ijengwe jimboni kwake , mwingine aligawa nyumba za serikali kwa mahawala,mwingine alihamishia gesi kutoka mtwara mpaka kwao bagamoyo, mwingine alijaza ndugu zake kila wizara alipooenda..mf, alipoenda uchukuzi akawajaza kabila lake bandarini,,,Wamesahau somo HAKI NA USAWA alilowaachia wamejaa..UBAGUZI NA UBINAFSI.

6. UWAJIBIKAJI NA UFUATILIAJI MAKINI...aliweza kufatilia ugawaji mahindi ya chakula kwa watendaji wabadhilifu na kuwajibisha hapo hapo..toka ameondoka HAKUNA UWAJIBIKAJI, HAKUNA UFUATILIAJI MAKINI..dawa japo chache hazifiki zinaishia pharmacy zao, Tembo wanauliwa ...hakuna anafailia!!, Madawa ya kulevya yanaingia na kutoka hakuna... anayejali!! Twiga wanapandishwa ndege..hakuna anayewajibishwa !!, nk nk..inauma kweli !!!
Tuna mshukuru MUNGU KAMTOA huko alikotaka kubadilisha mfumo, wakagoma kubadilika kwa maslahi yao binasfi. KAMLETA HUKU TUUNGANE NAE KUBADILI MFUMO MZIMA TUTENGENEZA TANZANIA MPYA. KWA MAFUAA YETU NA VIZAZI VYETU.
MUNGU ATUPE NINI ZAID WATZ, KAMA SIO HUYU MKOMBOZI...
MUNGU MBARIKI EDWARD NGOYAI LOWASSA!
MUNGU BARIKI TANZANIA!

/Vijimambo.

No comments :

Post a Comment