dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, September 11, 2015

Polisi wawatoa hofu watalii Zanzibar


By Haji Mtumwa, Mwananchi


Zanzibar. Polisi imewatoa wasiwasi wananchi wa visiwani hapa na watalii kutoka nchi ya nje ikisema itamarisha ulinzi na usalama katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame alitoa kauli hiyo katika mkutano maalum wa kujadili hali ya amani na utulivu Mkoa wa Kaskazini Unguja, jana.

Mkutano huo uliwajumuisha wawekezaji, viongozi mbalimbali wa mma na maofisa wa polisi nchini.

Makame alisema Polisi wamejiandaa kukabiliana na changamoto zitakazojitokeza katika kipindi hiki na baada ya uchaguzi huo.

“Wawekezaji mnapaswa kufahamu kuwa uchaguzi ni sehemu ya demokrasia tu, ila amani na utulivu kwa wenyeji na wageni itakuwapo wala msiwe na shaka,” alisema.

Kamishna Msaidizi wa Polisi, Hassan Msangi alisema baadhi ya watalii wanakabiliwa na hofu kutokana na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwezi ujao.Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wawekezaji wa Sekta ya Utalii Zanzibar, Omar Said alisema wanapanga mikakati ya kiusalama hususan katika maeneo ya biashara za kitalii ili kuwapa imani wawekezaji na wageni.

Mjumbe wa jumuiya hiyo na mmiliki wa Hoteli ya Mnarani Beach Cottages, Nassor Salum El-Mahruki alisema wawekezaji wamefarijika kwa kauli ya polisi kuhusu usalama wao.

No comments :

Post a Comment