Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, September 12, 2015

SCRUB YA KAHAWA NA MAFUTA YA NAZI KWA MIGUU

Wanawake wengi wanapenda kwenda saluni kuosha miguu na kusuguliwa lakini nia ni moja tu ya kuondoa ngozi iliyokufa na kuwa na ile laini.

Leo nakuletea scrub nzuri unayoweza kuitumia ukiwa nyumbani kwako na ikaifanya miguu yako kuwa na mvuto. Pia ina uwezo wa kuondoa ngozi ngumu.

Kwa wale wenye tatizo la kupasuka kwa miguu scrub hii husaidia kuitunza isipatwe na tatizo hilo.

Unaiandaaje?

Chukua mafuta ya nazi yanayoitwa virgin nusu kikombe, changanya na kahawa kiasi kisha weka vijiko viwili vya chai vya vanilla. Changanya kwa pamoja upate mchanganyiko wako.

Baada ya hapo andaa sabuni ya maji na maji ya vuguvugu, osha miguu yako mpaka itakate. Ukishamaliza chukua scrub yako, paka miguu na usugue kama unayefanya masaji. Kaa kwa muda wa dakika 10.

Scrub hii itaondoa ngozi yote iliyokufa na kukufanya ubaki na ile ya kuteleza. Kama una uwezo scrub hii ni nzuri sana kwa kutumia mwili mzima.
-GPL

No comments :

Post a Comment