Dar es Salaam. Watu kadhaa wamejeruhiwa, mmoja yuko mahututi na amelazwa kwa matibabu katika Hospitali ya Ndanda wilayani Masasi baada ya watu wenye silaha kuteka malori matano toka katika kijiji cha Nangoo kilichopo barabara kuu ya Mtwara- Masasi.
Utekaji huo umetokea usiku wa kuamkia leo ambapo licha ya madhara kwa binadamu watekaji hao wamepora fedha taslimu Shilingi milioni mbili na simu za mkononi kumi na tatu.
Kamanda wa Polisi mkoani Mtwara, Henry Mwaibambe akiongea na Mwananchi Digital kuwa majeruhi wa tukio hilo walipatiwa matibabu katika Hospitali ya Ndanda na kuruhusiwa isipokuwa mmoja ambaye hali yake ni mbaya.
Amesema watu hao walifunga barabara kwa magogo ili kusimamisha magari yaliyopita eneo hilo na kwamba walitekeleza utekaji huo kwa kutumia mapanga na marungu.
Kamanda Mwaibambe amesema polisi wameanza uchunguzi wa tukio hilo ili kuwabaini na kuwakamata wahusika ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.
No comments :
Post a Comment