dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, September 10, 2015

Abubakary Zubeiry achaguliwa rasmi Mufti Mkuu wa Tanzania

Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally. Picha ya Maktaba.
By Louis Kolumbia, Mwananchi Digital
Dar. Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) leo limemchagua Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally  kuwa Mufti Mkuu wa Tanzania.
Katika uchaguzi huo uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Africa Dream mjini Dodoma, Tume ya Dini ya Kiislamu imemchagua Sheikh Zubeiry kwa kura 310 za ndiyo baada ya kuingia kwenye uchaguzi huo akiwa mgombea pekee.
Akitangaza matokeo hayo, Mwenyekiti mstaafu wa Halmashauri Kuu ya Bakwata, Alhaji Habib Ndassiwa amewataja wagombea waliojitoa kuwa ni Sheikh Ally Muhidini Mkoyogole, Sheikh Hamis Abbas Mtupa na Sheikh Hassan Ibrahim Kiburwa.
Mufti Zubeiry aliteuliwa kukaimu nafasi hiyo ya juu katika dini ya Kiislamu mnamo Juni 22 mwaka huu baada ya kifo cha Mufti Issa Shaaban Simba kilichotokea katika Hospitali ya TMJ jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Alitakiwa kushikilia nafasi hiyo kwa muda wa miezi mitatu (Siku Tisini) hadi Septemba mwaka huu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa kujaza nafasi hiyo.

No comments :

Post a Comment