dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, October 19, 2015

JK ameteua Massawe Mkurugenzi Mkuu TPA.

Rais Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete, amemteua Awadh Massawe, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).
 
Rais Kikwete alitangaza uamuzi huo Ijumaa iliyopita wakati wa tukio la kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Bandari mpya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
 
Akihutubia wakati wa tukio hilo, Rais Kikwete alisema yeye alishamaliza uteuzi huo na kumwambia Massawe afuatilie tu barua yake rasmi ya uteuzi.
 
“Mimi nilishalimaliza hilo, fuatilia tu barua yako ya ajira,” alisema Rais Kikwete.
 
Kabla ya uteuzi huo, Massawe amekuwa akifanya kazi kama Kaimu katika nafasi hiyo tangu Febrfuari, mwaka huu na kufanikiwa hadi sasa kufanya mageuzi makubwa katika kuleta ufanisi katika bandari hapa nchini. 
 
Pia kabla ya kukaimu nafasi hiyo, Massawe alikuwa Meneja Bandari ya Dar es Salaam.
 
Baada ya kuwa Kaimu Mkurugenzi, alianzisha mikutano ya wadau yenye lengo la kurudisha mahusiano yaliyokuwa yameyumba kati ya pande hizo mbili.
 
Mikutano hiyo inayofanyika kila Alhamis ya mwisho ya kila mwezi, inalenga kuhusisha wadau mbalimbali katika majadiliano ya jinsi ya kuboresha ufanisi katika Bandari ya Dar es Salaam.Pia mwishoni mwa Juni, mwaka huu, TPA ilifungua ofisi ndogo katika mji wa Lusaka, Zambia.
 
Mafanikio mengine ya hivi karibuni ni kuanza kwa mfumo mpya wa malipo kwa njia ya mtandao katika Bandari ya Dar es Salaam.
 
Inatarajiwa kuwa baada ya kukamilika kwa ujenzi huo wa Bandari ya Bagamoyo utagharimu Dola bilioni 10 za Marekani, kutaongeza uwezo wa Bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara zinazohudumia tani milioni 12 za mizigo kwa mwaka, makasha 6,000 na kuajiri watu 3,200 na vibarua 1,500.
 
Bandari hiyo mpya inatarajiwa kuhudumia tani 600,000 za mizigo na makontena 1,000 kwa mwaka na kuajiri watu 1,000.
 
Awamu ya kwanza ya mradi huo itahusisha gati nne ambapo mbili kati ya hizo zitatumika kwa huduma ya makontena pekee, moja kwa ajili ya mizigo mingine.
 
Tayari TPA iko katika hatua za mwisho kulipa fidia kwa wanavijiji zaidi ya 2,000 walioachia ardhi yao kupisha mradi huo.
 
Mradi huo utatekelezwa kwa makubaliano ya pande tatu za Serikali ya Tanzania, China Merchants Holdings International (CMHI) ya China na State Government Reserve Fund (SGRF) ya Oman.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment