Mgombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Wananchi (Cuf), Maalim Seif Sharif Hamad amesema akichaguliwa kuwa rais atakuza uwezo wa serikali kujiongezea mapato na kuongeza kima cha chini cha mshahara hadi kufikia Sh. 400,000.
Akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni katika Uwanja wa Masumbani Jimbo la Chumbuni, Maalim Seif, alisema sera ya Cuf imeonyesha maeneo mengi ya kukuza uchumi na kuziba mianya inayochangia kupotea mapato ya serikali, hivyo hakuna kitakachozuia serikali kuwalipa wafanyakazi na wastaafu kiwango cha kuridhisha.
Alisema kwa upande wa askari wa vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, majukumu yao ni makubwa na magumu zaidi na kima cha chini watakacholipwa itakuwa ni Sh. 450,000 ambapo kwa upande wa wastaafu pencheni yao itaanzia Sh. 200,000.
Alisema hivi sasa uwezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni kukusanya Sh. bilioni 30 kwa mwezi, lakini kwa mipango ya Cuf kikichaguliwa kuongoza Serikali na kwa kutumia ilani yake ya uchaguzi, kitaongeza mapato hayo hadi kufikia Sh. bilioni 50 kwa kuanzia.
Katika hatua nyingine, Maalim Seif alisema kuwa akichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar, serikali yake itatoa elimu bure kuanzia msingi hadi chuo kikuu.
Alisema huduma za afya pia zitatolewa bure katika hospitali na vituo vyote vya afya vya serikali, ikiwa ni hatua ya kutekeleza malengo ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar, marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
“Hivi sasa viongozi waliopo wanasema wanalinda misingi ya Mapinduzi, lakini huduma nyingi wananchi wanalipishwa, mimi ndiye nitakaye vaa viatu vya mzee Karume,” alisema.
Mwenyekiti wa timu ya ushindi ya Cuf, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Nassor Ahmed Mazrui, alisema serikali itakayoundwa na Cuf iwapo wananchi watakichagua itaunda tume huru ya mipango itakayokuwa na uwezo mkubwa wa kubuni ya kuiondoa Zanzibar kwenye umasikini.
Alisema kuwa miradi mingi inayotekelezwa Zanzibar hivi sasa ni ya kutumia fedha badala ya kuingiza fedha, jambo ambalo linasababisha serikali kushindwa kukusanya mapato vizuri na kuweza kuwa na uchumi unaopaa kwa kasi.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments :
Post a Comment