Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, October 4, 2015

Lowassa avitahadharisha vyombo vya dola

Image result for LOWASSA

Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demekrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), amevionya vyombo vya dola kuacha tabia ya kuwapiga na kuwanyanyasa wafuasi wa Chama cha Wananchi (Cuf) na kwamba dawa ya kuondokana na manyanyaso hayo ni kutokipigia kura Chama cha Mapinduzi (CCM). 

Akihutubia umati wa wanachama na wafuasi wa Cuf katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Tibirinzi, Pemba, alisema hayo baada ya Maalim Seif Sharif Hamad, kutoa taarifa kwamba vyombo vya dola Zanzibar vimekuwa na tabia ya kuwapiga na kuwanyanyasa wanachama wa Cuf.

“ Nawaambia vyombo vya dola acheni tabia hiyo ya kuwapiga Cuf kuwapiga ni sawa na kuwapiga Ukawa,” alionya.

Akizungumza na wananchi na wafuasi Kisiwa cha Unguja, katika mkutano wa hadhara, uliofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja, alisema ana matumaini makubwa kuwa atawaongoza Watanzania na kushinda katika uchaguzi mkuu, kutokana na mapokezi makubwa anayoyapata kutoka kila mkoa.

Aliwataka wanachama wa Ukawa kuhakikisha wanadhibiti wizi wa kura na kulinda kura zao siku ya uchaguzi mkuu na kutobanduka katika masanduku ya kura.

“Naomba kura zenu kwani nahitaji kura nyingi za ziada maana hawa majamaa ni mahodari wa kuiba kura, hivyo mnipe kura nyingi sana za ziada hata kama wataiba ushindi niwe nao,” alisema.

Alisema endapo atapata ridhaa hiyo ya Watanzania atasimamia Muungano wa serikali tatu.

Naye mgombea urais wa Zanzibar kupitia Cuf,Maalim Seif, alimtahadharisha mgombea mwezake wa urais kupitia CCM, ambaye pia ni rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, kuhakikisha nchi inabaki katika amani hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Maalim Seif alisema kumekuwapo na taarifa zisizo na ukweli zilizotolewa na mgombea huyo pamoja na viongozi wengine wa CCM kuwa Cuf imeandaa vijana kwa ajili ya kufanya vurugu siku ya uchaguzi mkuu.

Alisema Cuf haina sababu ya kufanya fujo wala vurugu kwani wana uhakika na ushindi katika uchaguzi mkuu.

“Tafadhali Dk. Shein sema na balozi Seif Ali Iddi, makamu wa pili wa rais pamoja na Haji Omar Kheri, waziri wa nchi ofisi ya rais, idara maalum na vikosi vya SMZ, msiitie nchi katika machafuko kwani wewe ndiye utakaejulikana jiandae usije ukapelekwa katika mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai,” alisema.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment