Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, October 19, 2015

Magufuli aendelea kutikisa Mwanza!

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli.
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, ameendelea kutikisa mkoa wa Mwanza katika kampeni zake za lala salama kutokana idadi kubwa ya wananchi wanaojitokeza kumsikiliza kwenye mikutano yake.
 
Baada ya juzi kulitikisa jiji la Mwanza baada ya umati kujitokeza katika mkutano wake wa kampeni kwenye viwanja vya furahisha, mgombea huyo jana aliendelea kupata mapokezi makubwa kwenye majimbo mbalimbali ya mkoa huu ambayo alifanya mikutano yake ya kampeni.
 
Aidha, msafara wa Dk. Magufuli ulikuwa ukisimamishwa mara kwa mara na mamia ya wananchi wanaovamia barabara wakitaka azungumze nao kwenye maeneo mbalimbali alikopita akielekea kwenye mikutano yake.
 
Jana mgombea huyo alisimamishwa zaidi ya mara 10  kuanzia Mwanza Mabatini, Stendi ya Nyakato, Igoma, Kisesa, Nyanguge, Kahangara, Lugeye na Ilungu, ambako alizungumza na wananchi wa maeneo hayo akiwa njiani kuelekea kwenye mkutano mkubwa wilaya ya Magu.
 
AKERWA NA MITUMBA
Akizungumza na wakazi wa Jimbo la Magu, mkoani hapa, Dk. Magufuli aliwahakikishia wananchi kuwa, iwapo atashinda urais serikali yake italijali zao la pamba na ataweka mazingira mazuri yatakayowezesha lipande bei.Alisema haipendezi Watanzania kuendelea kuvaa mitumba wakati wanaweza kuendeleza zao la pamba na kuzalisha nguo za kuvaa wenyewe na kuuza nje ya nchi kuingiza fedha za kigeni.
 
Alisema serikali yake itajenga viwanda vingi kwa ajili ya kuongeza thamani ya zao hilo badala ya kuuza malighafi  nje ya nchi.
 
“Haiwezekani Tanzania yenye katani na pamba ikaendelea kuagiza mitumba kutoka nje…yaani sisi tunawauzia pamba wanatengeneza nguo wanazivaaa ndipo wanatuletea, lazima tubadilike tutumie pamba yetu kutengeneza nguo tuwauzie wao,” alisema. 
 
Alisema serikali yake itatoa dawa za pamba na pembejeo kwa wakati ili kuinua kilimo cha zao hilo na wakulima waweze kuuza kwa bei ya faida hali itakayowahamasisha wananchi wengi kulima zao hilo.
 
Aidha, alisema anajua wakazi wengi wa Kanda ya Ziwa ni wafugaji, hivyo ataanzisha viwanda vya bidhaa za mifugo na samaki ili wafugaji wanufaike na mifugo yao kwa kuuza kwa bei ya juu.
 
“Nilipokuwa Waziri wa Mifugo samaki waliongezeka sana kwasababu tulipambana na uvuvi haramu….wananchi tuache kuua mazalia ya samaki ili waongezeke watusaidie kwenye uchumi wetu,” alisema.
 
MSAFARA WASIMAMISHWA
Ukiwa njiani kuelekea Jimbo la Kwimba, msafara wa Dk. Magufuli ulizuiwa mara nane  na wananchi wa vijiji mbalimbali wakitaka kuzungumza na mgombea huyo.
 
Msafara huo ulisimamishwa kwenye vijiji vya Kabila, Maligisu, Kadesh, Kalalo, Sumve Mjini, Uwanja wa Ngudu, Nyamirama na Mngumarwa,ambako alisimama na kuzungumza na wananchi.
 
Akizungumza na wananchi wa Kwimba kwenye viwanja vya Ngudu, mgombea huyo alisema anataka kuwa Rais ili awatume  mawaziri kutekeleza miradi mbalimbali ya wananchi kwa ufanisi kama alivyokuwa anafanya.
 
Pia alisema serikali yake itapunguza bei ya vifaa vya ujenzi kama nondo, bati, misumari na saruji ili kuwawezesh wananchi wengi kumudu kuvinunua na kujenga nyumba bora za kuishi.
 
“Siwezi kuja hapa kuwadanyanganya kama wengine waliopita kwamba nitamaliza nyumba za tembe ndani ya siku 100…..hizo ni ndoto za mchana kwasababu huyo anayesema hivyo hata anakotoka hajazimaliza…..mimi nitawezesha kushuka kwa bei ya vifaa vya ujenzi ili wananchi wamudu kujenga nyumba bora,” alisema Dk. Magufuli.
 
AKERWA MGOGORO CCM 
Dk. Magufuli alisema migogoro ndani ya chama hicho wilaya ya Misungwi ndiyo imechelewesha maendeleo ya wilaya hiyo na kuwataka viongozi kuacha tofauti zao.
 
Alisema migogoro hiyo pia imekuwa ikidhoofisha chama hicho na kutoa mwanya kwa wapinzani kuitukana serikali kwamba haijafanya lolote.
 
“Msimkaribishe shetani, nataka muwe wamoja na kuanzia leo (jana) nataka mwende mkafanyiane kampeni, mbunge wafanyie kampeni madiwani na madiwani mumfanyie kampeni mgombea ubunge, mgawanyiko na malumbano yenu haiwezi kuisaidia Misungwi,” alisema.
 
Aidha, Dk. Magufuli alisema ameamua kusema ukweli kuhusu malumbano ya viongozi hao kwa kuwa yeye ni mtu wa kazi na hapendi kuona viongozi wakishindia malumbano badala ya kutatua kero za wananchi.
 
“Najua kuna wengine hapa mchana CCM usiku upinzani, sasa hayo hayatawasaidia, muwe kitu kimoja kuhakikisha CCM inashinda, iwekeni Misungwi mbele na muachane kabisa na malumbano,” alisema. 
 
BULEMBO
Akizungumza kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Abdalah Bulembo, alisema kuondoka ndani ya chama hicho kwa mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombare Mwiru hakuwezi kukitikisa chama hicho.
 
Alisema chama hicho kina hazina kubwa ya wazee ambao hawajawahi kuhama kwenye chama hicho na walio hai wameendelea kuwa washauri wazuri.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment