Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli amepata mapokezi ya kifalme mkoani Mwanza kufuatia umati wa wananchi waliojitokeza kumpokea alipowasili kwa mara ya kwanza mkoani hapa jana kwa ajili ya kampeni za lala salama.
Mgombea huyo aliwasili jana saa nane mchana kwa ndege akitokea jijini Dar es Salaam na kukuta uwanja wa ndege ukiwa umefurika idadi kubwa ya watu, wengine wakiwa wamejipanga barabarani.
Wananchi walijipanga barabarani kuanzia Uwanja wa Ndege wa Mwanza hadi viwanja vya Furahisha, ulipofanyika mkutano wa hadhara na kusababisha msongamano mkubwa.
Watu wa usalama walifanya kazi ya ziada kupangua watu barabarani ili msafara wa mgombea huyo upite kutokana na umati huo uliotaka kumuona.
MBWEMBWE ZATAWALA
Mapokezi hayo ya Dk. Magufuli yalitawaliwa na kila aina ya mbwembwe na burudani kwani watu walijitahidi kufanya vituko kuonyesha mapenzi yao kwa mgombea huyo.
Wanawake waliompokea uwanja wa ndege waliunganisha vipande vya kanga na kupanga barabarani ambapo msafara huo ulipita huku wengine wakionekana wakifagia na kupiga deki barabara hiyo.Mgombea huyo aliwasili jana saa nane mchana kwa ndege akitokea jijini Dar es Salaam na kukuta uwanja wa ndege ukiwa umefurika idadi kubwa ya watu, wengine wakiwa wamejipanga barabarani.
Wananchi walijipanga barabarani kuanzia Uwanja wa Ndege wa Mwanza hadi viwanja vya Furahisha, ulipofanyika mkutano wa hadhara na kusababisha msongamano mkubwa.
Watu wa usalama walifanya kazi ya ziada kupangua watu barabarani ili msafara wa mgombea huyo upite kutokana na umati huo uliotaka kumuona.
MBWEMBWE ZATAWALA
Mapokezi hayo ya Dk. Magufuli yalitawaliwa na kila aina ya mbwembwe na burudani kwani watu walijitahidi kufanya vituko kuonyesha mapenzi yao kwa mgombea huyo.
Baadhi ya vijana walioshikwa na mihemko walionekana wakienda mbele ya gari la Dk. Magufuli na kupiga ‘push up’ huku wengine wakijilaza barabarani hali iliyowafanya wana usalama kufanyakazi ya ziada kuwaondoa.
Vijana wengine walijilaza mbele ya gari la mgombea huyo kiasi cha kuhatarisha maisha yao hali iliyosababisha wakati mwingine msafara huo kusimama ili waondolewe.
Msafara huo ulisimamishwa mara kadhaa na wananchi waliovamia barabarani wakitaka msafara usimame na azungumze nao hali iliyosababisha msongamano mkubwa sehemu zote alizopita kuelekea viwanja vya Furahisha.
Dk. Magufuli akishangazwa na mapokezi hayo, alielezea furaha yake na kusema mikoa yote aliyopita alipata mapokezi makubwa lakini ya Mwanza yametia fora kutokana na wananchi kujaza uwanja huo kiasi cha wengine kupanda juu ya miti na kwenye paa za nyumba ili kushuhudia mkutano huo.
“Kwa kweli wananchi wa Mwanza mmenishangaza sana kwa mapokezi haya makubwa, ingawa kote nilikopita ni hivi hivi, lakini nyinyi mmetia fora…na si kwamba mmetia fora kwa Tanzania tu na Afrika nzima mapokezi kama haya hayajawahi kutokea,” alisema.
Akionyesha furaha yake, alisema mapokezi hayo yanamfanya aondoke na deni kubwa la kuwatumikia Watanzania na kuwaahidi akishinda nafasi ya urais ataugeuza mji wa Mwanza kuwa Geneva ya Afrika kwa maendeleo.
Alisema ameomba urais kuwatumikia Watanzania wote bila kujali vyama vyao vya siasa hivyo aliwaomba wakazi wa Kanda ya Ziwa kumpa ushindi wa kishindo siku ya kupiga kura.
“Naahidi kufanyakazi usiku na mchana kulipa deni maana mapokezi haya yamenishangaza …yaani kwa hali hii nichaguliwe halafu nishindwe kufanyakazi kweli, nipeni urais muone nitakavyowafanyia kazi maana mimi sijaomba urais kwa majaribio nina uzoefu wa kutosha,” alisema Dk. Magufuli.
Alisema ataufanya uwanja wa ndege wa Mwanza kuwa wa kimataifa hali ambayo itavutia wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali duniani kuwekeza katika sekta mbalimbali na kuinua kipato cha wananchi wa mkoa huo.
Alisema kuwa anataka Tanzania iwe na viwanda vya kutosha vitakavyosaidia kukuza uchumi kwa kasi na kuongeza nafasi za ajira kwa vijana Watanzania wasomi ambao wanamaliza vyuo na kukosa ajira.
Aliahidi Mwanza kujengwa mtambo wa umeme wa Kilovotli 400 ili kuvutia uwekezaji kwenye viwanda vya uzalishaji.
Alisema wenye viwanda kama kile cha Tannaries kilichoko Ilelema mkoani hapa ambao hawajaviendeleza wajiandae maana atawanyang’anya mara tu atakapoingia Ikulu.
“Mwenye hiki kiwanda kama amenisikia na yeye na mke wake wanataka kuninyima kura na waninyime, maana wana-Mwanza wote na Watanzania wengine wameshaamua kunipa kura,” alisema na kuufanya umati uliokuwa ukimsikiliza kumshangilia.
Alisema Rais Jakaya Kikwete aliwahi kuahidi kununua meli kubwa itakayofanya kazi katika Ziwa Victoria na kwamba ahadi hiyo yeye ndiye atakayeitekeleza. Aliwaahidi pia kujenga daraja la Kigongo mpaka Busisi ili wananchi wanaovuka wasilazimike kusubiri kivuko.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mwanza, Antony Diallo, alisema watu hao wamekuja wenyewe hawajakusanywa kwa mabasi.
Alisema sehemu ya umati huo kwa hiyari yao wamekesha kwenye viwanja hivyo wakiwa na shauku kubwa ya kumsikiliza yeye Magufuli.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments :
Post a Comment