Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, October 2, 2015

Ndege ya JWTZ yaanguka, marubani wapotea

  •  Msemaji wa JWTZ, Kanali Ngemela Lubinga alisema jana kuwa jeshi hilo linaendelea kuwatafuta kwa ushirikiano wa vyombo vya majini na anga.
By Mwandishi Wetu, Mwananchi
Dar es Salaam. Askari wawili wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wamepotea katika Bahari ya Hindi baada ya ndege waliyokuwa wakiitumia kwa mafunzo kuanguka jana.
Msemaji wa JWTZ, Kanali Ngemela Lubinga alisema jana kuwa jeshi hilo linaendelea kuwatafuta kwa ushirikiano wa vyombo vya majini na anga.
Kanali Lubinga alisema ndege hiyo ya mafunzo ilianguka saa 3.30 asubuhi eneo la Kisiwa cha Mbudya, kilichopo umbali wa mita 300 kutoka Hoteli ya Silversands, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Aliwataja wanajeshi hao kuwa ni; Luteni Kanali Kilikisa Ndongoro na Kapteni Gaudence Khamis ambao wote kwa pamoja walifanikiwa kuruka kwa parachuti kutoka ndani ya ndege hiyo lakini hawakufanikiwa kujiokoa na wakati wanaruka, wakatumbukia Bahari ya Hindi.
Alisema wanajeshi hao walikuwa kwenye mafunzo maalumu ya kurusha ndege za kijeshi kwa kutumia ndege maalumu za mafunzo.
“Chanzo cha ajali hiyo kilichangiwa na injini kupata hitilafu ikiwa angani na walijaribu kujiokoa lakini walipotumbukia bahari walipotea, walijaribu kuogelea lakini baadaye wakapotea na kazi ya kuwasaka inaendelea. Kuna helikopta ya polisi na meli za kijeshi za majini zinaendelea na kazi hiyo, Watanzania tunawaomba kuwa na uvumilivu katika tukio hilo,” alisema.
Wanajeshi wengine sita wafariki katika ajali
Katika tukio jingine, Wanajeshi sita wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Kambi ya Bulombola wamekufa na wengine 21 kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wanasafiria kupinduka jana.
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, Ferdinand Mtui alisema ajali hiyo ilitokea jana saa 10 jioni katika Mlima Pasua uliopo kati ya Wilaya ya Uvinza na Kigoma Mjini.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Maweni mkoani Kigoma, Fadhil Kibaya alisema amepokea maiti wanne na majeruhi wengine wawili walifariki dunia walipokuwa wakihudumiwa.

No comments :

Post a Comment