Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, October 3, 2015

NEC yashusha rungu kwa vyama vya siasa!

Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva
By Daniel Mjema,Mwananchi
Moshi.  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetoa muda wa saa 48 kwa vyama vya siasa vilivyobandika picha za wagombea maeneo yasiyostahili Jimbo la Moshi mjini kuyaondoa mara moja.
Agizo hilo lilitolewa jana na mwenyekiti wa kamati ya maadili ambaye pia ni msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo hilo, Shaban Ntarambe ambaye alisema hadi kufikia kesho ziwe zimeondolewa.
Hata hivyo Agizo hilo litaviathiri zaidi vyama vya upinzani kutokana na mabango mengi ya wagombea wao kubandikwa sehemu zisizostahili ukilinganisha na ya mgombea ubunge wa CCM, Davis Mosha.
Wakati picha za wagombea wengi wa upinzani zikiwa zimebandikwa hadi kwenye milingoti ya umeme na simu, picha za Mosha zimebandikwa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya matangazo ya biashara.
Sambamba na wagombea ubunge wa vyama vya upinzani, lakini kwa sehemu kubwa picha za wagombea Udiwani katika kata mbalimbali, baadhi yake zimebandikwa maeneo yasiyostahili.
Agizo la kuondoa mabango na vipeperushi maeneo yasiyoruhusiwa limetolewa na msimamizi wa uchaguzi wa Jimbo hilo, Shaban Ntarambe katika barua aliyowatumia makatibu wa vyama vya siasa.
Katika barua yake ya Oktoba 2, yenye kumb MMC/A.40/48/Vol.XXV/117, Ntarambe kwenda kwa makatibu wa vyama vya siasa, agizo lake linatokana na maazimio ya kamati hiyo ya Septemba 30.
Kufuatia agizo hilo, Kaimu Katibu mwenezi wa Chadema katika jimbo hilo, Mohamed Ally alisema agizo hilo linalenga kuvikandamiza vyama vya upinzania ambavyo havina uwezo kununua maeneo.

No comments :

Post a Comment