TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR INAWATANGAZIA WANANCHI WOTE WA ZANZIBAR KWAMBA KUANZIA TAREHE 19/10/2015 ITASITISHA ZOEZI LA UCHUKUAJI WA SHAHADA ZA KUPIGIA KURA KATIKA AFISI ZA TUME ZA WILAYA KWA UNGUJA NA PEMBA.
TUME INAWATAKA WALE WOTE AMBAO HAWAJACHUKUA SHAHADA ZAO KATIKA OFISI ZA TUME ZA WILAYA KUHARAKISHA KUCHUKUWA SHAHADA ZAO, KWANI ZOEZI LA UTOAJI WA SHAHADA HIZO KATIKA AFISI ZA WILAYA LITASITISHWA IFIKAPO TAREHE 19/10/2015, NA LITAENDELEA KUFANYIKA MAKAO MAKUU YA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR YALIYOPO MAISARA KWA UPANDE WA UNGUJA NA OFISI NDOGO YA UCHAGUZI YA ILIYOPO CHAKECHAKE PEMBA. HADI LITAKAPOTOKA TANGAZO JENGINE.
AIDHA TUME INAWAOMBA WANANCHI KUZINGATIA MUDA ULIOTOLEWA WA UCHUKUWAJI WA SHAHADA ZA KUPIGIA KURA KATIKA OFISI ZA WILAYA KWA LENGO LA KUONDOA USUMBUFU UTAKAOWEZA KUJITOKEZA.
TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR INAOMBA MASHIRIKIANO KWA KULIFANIKISHA ZOEZI HILI.
PIGA KURA KWA AMANI UPATE MAENDELEO NCHINI.UJUMBE HUU UMELETWA KWENU NA TUME YA UCHAGUZI YA ZANZIBAR.
/Zanzibar Human Rights Facebook
No comments :
Post a Comment