dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, October 16, 2015

Tunahimiza matumizi mazuri ya Kituo cha Mawasiliano cha Nec.

NA EDITOR

16th October 2015.

Katuni.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) hivi karibuni iliwataka wananchi kutumia vizuri kituo chake cha mawasiliano ambacho imekianzisha hivi karibuni kwa ajili ya kupata taarifa mbalimbali kuhusiana na uchaguzi mkuu.
 
Kituo hicho ambacho kimeanzishwa kwa ushirikiano na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kina lengo la kusaidia mawasiliano baina ya Nec na wapiga kura.
 
Ni mategemeo yetu kuwa kuanzishwa kwa kituo hiki kutaisaidia kwa kiasi kikubwa kuendeshwa kwa ufanisi kwa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.
 
Kumekuwa na malalamiko mengi ya kiutendaji kutoka kwa wapiga kura kabla ya uchaguzi kufanyika, hivyo tunaamini kwa kiasi kikubwa kituo hiki kitasaidia utatuzi wa matatizo haya. Kuna masuala mengi, ambayo wapiga kura watanufaika nayo kama kufahamu masuala mbalimbali yanayohusu upigaji kura kwa kuwasiliana na kituo hiki.
 
Tunapongeza Nec kwa hatua ya kuanzishwa kwa kituo hiki kwani uchaguzi wa mwaka huu unatazamiwa kuwa wa kihistoria na wenye ushindani mkubwa kutokana na ukweli kuwa kuna wapiga kura wengi wakiwamo vijana ambao wanashiriki kwa mara ya kwanza katika uchaguzi.Pia mwaka huu kumeshuhudiwa kuwa na ushindani mkali baina ya vyama, ambapo kwa mara ya kwanza itakuwa vigumu kutabiri chama kipi kitaibuka mshindi.
 
Kwa maneno mengine katika uchaguzi wa mwaka huu, kila kura ni muhimu, ndio maana hatua ya tume ya kuwa na kituo kama hiki itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza manung’uniko katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na baada ya uchaguzi huo.
 
Kutokana na kuwapo kwa kundi kubwa la wapiga kura, ni jambo sahihi kuwa na vituo vya aina hii kwani kutarahisisha pia kuelimisha watu taratibu za upigaji kura na mambo mengine muhimu. Tayari kuna malalamiko kuwa baadhi ya majina ya watu kutokuwapo kwenye orodha ya wapiga kura, sasa ni mategemeo yetu kuwa viongoni wa tume watafanyia kazi tatizo hilo. Kwani suala ya kupiga kura ni haki ya kikatiba kwa Watanzania, itakuwa jambo zuri kwa Nec kumaliza matatizo kama hayo. Uchaguzi wa mwaka huu unatazamiwa kuwa na changamoto nyingi, ukizingatia kuna ongezeko kubwa la wapiga kura lakini pia hamasa kubwa miongoni mwa wananchi ya kushiriki kwenye uchaguzi imeongezeka pia.
 
Watu waliojiandikisha kwenye Daftari la Wapiga Kura kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ni milioni 22.7.
 
Hii ni ishara tosha kuwa uchaguzi wa mwaka huu hautakuwa jambo dogo, ndio maana kunahitajika maandalizi kamambe ya  tume. Hata hivyo, tunatoa tahadhari kwa wananchi kukitumia kituo hiki vizuri kwani haitakuwa na maana kuwapo kwake halafu wananchi hawatakitumia vizuri chombo hiki.
 
Aidha, watu wanapaswa kujiepusha kutumia lugha za matusi kwani kituo hiki kinatakiwa kuwa daraja kati ya Nec na wapiga kura. Hata hivyo, wafanyakazi wa Nec nao wanapaswa kujiepusha na lugha zisizo za kiungwana kwa wapiga kura ili kuepusha matatizo yasiyokuwa ya lazima.
 
Pia tunaomba tume itangaze habari za kituo hiki ili wapiga kura wafahamu juu ya kuwapo kwake. Ni vizuri NEC ingetumia njia mbalimbali ili kuhakikisha namba za kituo hiki zinawafikia wapiga kura katika mikoa yote ya Tanzania.
 
Wakati tukihimiza matumizi mazuri ya kituo hiki, tunaomba viongozi na wafanyakazi wa Nec kutoa ushirikiano mzuri ili kufanikisha kazi za kituo hiki.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment