dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, October 16, 2015

UKAWA WAIBUA MADUDU 17 DAFTARI LA KURA!

  Waitaka Tume ya Uchaguzi (Nec) kuacha mchezo na daftari hilo kwa kuwa kufanya hivyo ni kutaka kusababisha machafuko nchini.

Mgombea urais wa Chadema anayeungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa, akihutubia katika mkutano wa kampeni kwenye Uwanja wa Shule ya Sabasaba wilayani Magu, mkoa wa Simiyu jana. Picha: Mpigapicha Wetu
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umeibua madudu 17 katika Daftari la Kudumu la Wapigakura.
 
Baadhi ya kasoro hizo 17 ni pamoja na picha za kivuli, hoteli, kontena, kivuli, raia wa kigeni kuandikishwa zaidi ya mara moja na picha za kujipiga.
 
Ukawa inaundwa na vyama vya Chadema, CUF, NCCR- Mageuzi na NLD, ambavyo kwa pamoja vimemsimamisha mgombea urais wao, Edward Lowassa, kwa tiketi ya Chadema.
 
Mkurugenzi wa Kampeni za Uchaguzi wa Chadema, Reginald Munisi, alizitaja kasoro hizo jana katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
 
Munisi alisema kasoro zilizopo zinaonyesha kuwa daftari hilo halijakamilika.
 
Alisema kasoro hizo ziligundulika katika kituo cha mpigakura cha Ofisi ya Kitongoji Azimio 1 chenye namba 10101010102, kilichopo mtaa wa Mahoma/Makulu, Kata ya Chahwa, Jimbo la Dodoma Mjini.
 
Alifafanua kuwa kasoro hizo ni pamoja na majina yasiyoeleweka kama mtu mmoja mwenye sura kama Mchina kuwa na jina la DHKAKJOHF KJSHFKJA KJHSOKJHS, wengine ni wale waliojipiga picha wenyewe na jina lake kusomeka ni GGGHUG.
 
Mwingine ni aliyejipiga picha mwenyewe ambaye ni mwanamke, lakini amepewa jina la Isack Obadia Mugassa na jinsia yake ni mume, mwingine ni mzungu ambaye ametokea mara mbili kwa picha za kujipiga mwenyewe, mwenye jina la Johan Peterse.

Picha nyingine ni ukuta ambao umepewa jina la Kabura Kiloloma Shaban na kupewa jinsia ya kike, nyingine ni picha ya mgahawa ambao umepewa jinsia ya kiume na jina la KJHBNLH BJHEN JHBNLH, mwingine ni mwenye picha ya kujipiga mwenyewe huku jina likiwa ni LHGFCJHSF JHGHJGF JGFHGF.Nyingine ni aliyejipiga picha kwa mbele katika sehemu yenye mwanga na jina lake kutokea kama MHMBKJB, mwingine mwenye jina QWE ASDF ZXCVB na mwingine QWERTYU QWRTY RTY na nyingine ni picha ya hoteli iliyopewa jinsia ya kiume na jina QWERTYU WERTYUI WERTYUO.
 
Kasoro nyingine ni picha ya ghala na kupewa jina la Zakayo Kigunga Richadi, huku nyingine ikiwa ni paa la bati lenye jinsia ya kiume na halina jina na kivuli chenye jinsia ya kike na hakina jina.
 
Munisi alisema inashangaza ilikuwaje watu waandikishwe zaidi ya mara moja kwa majina tofauti na kwamba mtu kama mzungu ni rahisi kumtambua, lakini kaandikishwa mara mbili.
 
“Wametupa daftari jana (juzi), lakini kwa muda mfupi tumegundua kasoro 17, tunashindwa kuelewa ni uchakataji gani uliofanyika hadi kutupa daftari hili kuwa limekamilika? alihoji. 
 
Aidha, waliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kuacha mchezo na daftari hilo kwa kuwa kufanya hivyo ni kutaka kusababisha machafuko nchini na uchaguzi usio huru na haki.
 
Akijibu madai hayo, Mkurugenzi wa Daftari la Kudumu na Tehama wa Nec, Dk. Modest Kipilimba, alisema mfumo wa kielektroniki wa Biometric Voters Registration (BVR), ni mara ya kwanza kutumika nchini na waliofanya kazi hiyo ni vijana wa Kitanzania ambao wameutumia kwa mara ya kwanza.
 
“Hayo makosa ni ya kibinadamu, mengi tumeyasahihisha na kuondoa visivyohusika, siyo kazi rahisi kabisa, ndiyo maana tumewapa vyama vya siasa waliangalie ili nao watusaidie,” alisema na kuongeza:
 
“Duniani kote huwezi kukwepa makosa, ni makosa  ya kibinadamu...tukumbuke ni mara ya kwanza mfumo huu kufanyika hapa nchini, tunafanyia kazi kwa haraka makosa hayo na tutayaondoa,” alisema.
 
Alipoulizwa iwapo makosa hayo kama yanaweza kuathiri idadi ya wapiga kura milioni 22.7 iliyokwishatolewa na Nec, alisema upo uwezekano wa idadi ya wapiga kura kupungua kwa kuwa kuna majina ambayo yataondolewa.
 
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bara, Profesa Abdalah Safari, alikunzumza kwa niaba ya Ukawa, aliitaka Nec kuliweka wazi daftari hilo kwa mujibu wa sheria ili wananchi waone taarifa zao, huku akiwataka wananchi kujitokeza kuangalia majina yao na kutoa taarifa wanapobaini kasoro.
 
Undikishaji wa wapigakura kwa mfumo wa BVR, ulianza Februari na hadi Agosti, mwaka huu, watu milioni 23.8 waliandikishwa.
 
Hata hivyo, baada ya Nec kuchakata dafatari hilo, watu milioni 22.7 ndiyo waliothibitika kuwa wapigakura halali.
 
Kwa mujibu wa sheria, baada ya Nec kukamilisha daftari,  inapaswa kuvipa vyama vya siasa na baadaye hubandikwa katika vituo vya kupigia kura kwa ajili ya wananchi kuona taarifa zao.

CHANZO: NIPASHE




 



No comments :

Post a Comment