Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, November 10, 2015

Dk Shein, Maalim Seif, marais wateta Zanzibar!


By Hassan Ali, Mwananchi
Zanzibar: Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk Mohamed Shein na mwenzake wa ya CUF, Maalim Seif Sharrif Hamad jana walikutana kwa faragha kwa takriban saa tano, lakini hakuna taarifa iliyotolewa kuhusu kilichojadiliwa kwenye kikao hicho.
Kikao hicho, ambacho pia kiliwahusisha marais wastaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano, Ali Hassan Mwinyi na Amani Karume, kimefanyika katika kipindi ambacho kuna hali ya sintofahamu visiwani hapa tangu Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha atangaze kufuta matokeo ya uchaguzi wa Rais na wawakilishi.
Jecha, ambaye alifuta matokeo hayo siku chache baada ya Maalim Seif kujitangazia ushindi, aliahidi kuitisha uchaguzi mpya ndani ya siku 90, lakini CUF imesema haitashiriki.
Kikao kilichofanyika Ikulu ya Mnazi Mmoja mjini hapa, kilianza saa 4.15 asubuhi na kumalizika saa 9.40 mchana.
“Ikulu ilikuwa tulivu hakuna kilichoonekana kuongeza harakati licha ya vizuizi vya kamba vilivyokuwa vimezungushwa tangu ulipomalizika uchaguzi,” alisema mmoja wa maofisa watendaji wa ofisi hiyo ya Rais.
Hii si mara ya kwanza kwa wawili hao kukutana tangu kumalizika kwa uchaguzi ulioiweka Zanzibar njia panda baada ya ZEC kuamua kutoendelea kutangaza matokeo.
Hata hivyo, inaonekana ni mara ya kwanza kwa wagombea hao kukaa meza moja na safu kubwa ya viongozi hao wa kisiasa na maongezi yao kuchukua muda mrefu.
Mkutano huo umefanyika siku moja baada ya Maalim Seif kukutana na watendaji wa kamati za utendaji za matawi na wilaya wa Unguja na pia jana kuongea na viongozi wa ngazi hizo kwa upande wa Pemba.
Katika vikao hivyo, Maalim Seif amekuwa akisisitiza wafuasi kuendelea kuwa watulivu huku akiahidi kuendelea kupigania haki yake.
Katika hatua nyingine, wajumbe wateule 27 wa Baraza la Wawakilishi kutoka CUF wameitaka ZEC kutengua tamko la mwenyekiti wake la kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu kwa madai kuwa ni kinyume na Katiba na sheria za Zanzibar.
Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wawakilishi hao 17 kutoka kisiwani Pemba na tisa kutoka Unguja walisema wameamua kutoa msimamo huo baada ya ZEC kukaa kimya wakati ikitambua kuwa mwenyekiti wake amevunja Katiba na sheria ya Zanzibar na kuviingiza visiwa hivyo katika mgogoro usiokuwa na msingi.
“Tumeamua kuja hadharani na kuitaka ZEC kutengua tamko batili la mwenyekiti wake na kukamilisha majumuisho ya kura za urais wa Zanzibar ili rais mpya atangazwe na kuitisha baraza jipya la wawakilishi lililochaguliwa Oktoba 25 kwa mujibu ya Katiba ya Zanzibar ili sisi na wenzetu wa CCM tuweze kuapishwa na kuanza kutekeleza majukumu yetu ya kuwatumikia wananchi waliotuchagua,” alisema aliyekuwa mwakilishi wa Mgogoni, Aboubakar Khamis Bakary aliyezungumza kwa niaba ya wenzake.
Bakary alisema uchaguzi wa wawakilishi na madiwani ulikuwa umekamilika na washindi kutangazwa kwa majimbo na kata zote za Unguja na Pemba.
“Wagombea tulioshinda kutoka vyama vyote tulishapewa rasmi hati za uthibitisho wa kuchaguliwa na wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo… na leo tumekuja na nakala za taarifa rasmi ambazo kila mmoja wetu alipewa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo lake kuthibitisha kuchaguliwa kwake,” alisema.
Alisema Sheria ya Uchaguzi ya Zanzibar, kifungu cha 123, imeweka bayana kwamba baada ya msimamizi wa uchaguzi kumtangaza mshindi, nafasi pekee ya mtu mwenye malalamiko kutaka matokeo yatenguliwe ni kwa kufungua kesi Mahakama Kuu ya Zanzibar.
Alisema haiingii akilini kwa ZEC kuyatambua matokeo ya wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanaotokea majimbo ya Zanzibar wakati uchaguzi huo na ule wa wawakilishi ulifanyika siku moja wakati mmoja na kutumia daftari moja la wapigakura.
“Utawezaje kusema uchaguzi wa wabunge wa Zanzibar ulikuwa halali na usio na dosari na wakati huo wa wawakilishi haukuwa halali na ufutwe? ” alisema.

No comments :

Post a Comment