Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, November 3, 2015

Kada wa CCM apalilia ushindi wa Dk. Magufuli.

Dk. John Magufuli.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Singida, Aysharose Mattembe, amesema ushindi wa Dk. John Magufuli (pichani), ni ishara kuwa Watanzania wanataka mabadiliko ya maendeleo na si bora mabadiliko.
 
Amesema ana imani kubwa Watanzania hawatajutia uamuzi wala kura zao walizompigia Dk. Magufuli kwa kuwa yote aliyoahidi yanakwenda kufanyiwa kazi na hatimaye Tanzania kuwa ya tofauti katika muda mfupi ujao. Aidha, amesema uchaguzi umemalizika kwa amani na Watanzania wamefanya uamuzi, kilichobaki ni wote kuungana na kufanya kazi kwa bidii ili kuleta mabadiliko yanayokusudiwa.
 
Aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa kutoa shukrani zake kwa Watanzania na wananchi wa Singida kwa kumchagua Dk. Magufuli na wagombea ubunge na udiwani wa CCM.
 
Alisema wananchi wa Singida wameonyesha mshikamano mkubwa na ukomavu wa kisiasa kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mikutano ya hadhara kusikiliza sera na baadaye kufanya uamuzi sahihi wa kuwachagua wagombea wa CCM.
 
“Niko hapa kuwashukuru Watanzania wote kwa kufanya uamuzi sahihi wa kumchagua mgombea urais wetu, Dk. John Magufuli,” alisema. “Uamuzi waliofanya umetokana na CCM kumsimamisha mtu makini, mwadilifu na mwenye dhamira ya dhati ya kutuletea maendeleo ya haraka na ya kweli. Kazi kubwa iliyopo mbele yetu ni kuungana na kufanya kazi kwa bidii kutimiza ndoto za Watanzania. Falsafa yetu ya `Hapa kazi tu’ ndiyo inakwenda kutekelezwa sasa,” aliongeza Aysharose.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment