Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na Nipashe kuhusu maandalizi ya kuwapokea wageni mbalimbali kutoka nje ya nchi wanaotarajia kuhudhuria sherehe hiyo.
“Mialiko imeshakwenda, lakini mpaka sasa hakuna aliyewasili, ila tumeshaanza kupokea majibu ya viongozi mbalimbali wa kanda kuwa watafika katika sherehe hiyo,” alisema Balozi Mulamula.
Alisema nchi jirani kama Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Uganda, zimethibitisha kushiriki sherehe za kumuapisha Dk. Magufuli. Alisema orodha kamili na idadi ya wageni watakaokuja, bado haijapatikana, lakini Wizara imeshajiandaa kupokea idadi yoyote ya wageni watakaokuja.Alisema licha ya Ofisi ya Waziri Mkuu kusimamia sherehe hiyo, lakini Wizara nayo imejipanga katika suala zima la malazi kwa wageni watakaofika nchini.
Aliongeza kuwa pia wanatarajia kupokea wageni kutoka China, nchi za Nordic, Marekani na Uholanzi.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment