AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, November 30, 2015

Makamanda UVCCM watakiwa kutokiangusha chama chaguzi.

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka.
Makamanda wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), wametakiwa kuwa mstari wa mbele kukipigania chama chao na kuhakikisha  kinapata ushindi katika kila uchaguzi mkuu Tanzania Bara na Zanzibar. 
 
Akizungumza na makamanda wa UVCCM wa mikoa, wilaya, majimbo na wadi, huko Kilimani, mkoa wa Mjini Magharibi jana, Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka, alisema jukumu kubwa la makamanda hao ni  kupigana vita ya kisiasa na atakayeshindwa atakuwa ameshindwa kutumikia ukamanda  wake vizuri, hivyo kukiangusha chama.  
 
Alisema si jambo jema kwa makamanda kutoshirikishwa wakati wa uchaguzi, lakini pia si sawa wakajiweka nyuma wakati wa mapambano ya kutafuta kushinda uchaguzi ili kukamata dola. 
 
 “Nimekuiteni ili kuwakumbusha majukumu yenu, bila nguvu zenu, mipango na mikakati yetu ni vigumu kushinda vita iliyo mbele yetu, msibaki nyuma pambaneni hadi ushindi upatikane,” alisisitiza.
 
Aidha, Shaka aliwataka viongozi wa wadi, majimbo, wilaya na mikoa kuwapa ushirikanao makamanda hao, kwa sababu ndiyo wanaowajua vijana hodari, makini na shupavu wanaoweza kuhimili dhoruba za kisiasa wakati wa uchaguzi.“Mapinduzi ya mwaka 1964 kulikuwa na kikosi cha makamanda 14 waliopanga ramani ya mapambano baadaye wakaungwa mkono na makamanda wengine kuuangusha utawala wa mfalme mvamizi aliyeikalia Zanzibar kinyume na haki. Kama wenzetu 14 waliweza iweje sisi kikosi cha makamanda  400,000 wa UVCCM baada ya miaka 52 ya Mapinduzi tushindwe?, tunaweza na tutashinda vita hii tujipange vizuri,” alisema. 
 
Shaka alisema makamanda wa CCM wana hadhi na daraja kubwa mbele ya chama na kila mmoja anatambua umuhimu wao, hivyo wanatakiwa kudhihirisha umuhimu wao kwa kukisaidia chama kushinda chaguzi mbalimbali. 
 
Aliwataka makamanda wa CCM kukutana na kupanga mbinu na mikakati ya kukabili vita ya kisiasa na kumpelekea ili aibariki kabla ya uanza operesheni kuelekea ushindi uchaguzi wa Zanzibar na  kulinda mapinduzi. 
Aliwahimiza makamanda hao kuwa na umoja, upendo, kutunza siri za chama na kuaminiana ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
 
Kwa upande wao, makamanda hao walimuahidi Kaimu Katibu Mkuu huyo wa UVCCM ushiriki wao  wa dhati katika uchaguzi wa marudio Zanzibar unatarajiwa kufanyika mara baada ya kutangazwa na Tume ya uchaguzi ya visiwa hivyo (Zec) ili CCM iweze kupata ushindi mkubwa.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment