Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, November 7, 2015

Marekani yamtaka Magufuli kumaliza mgogoro Zanzibar!

Dar es Salaam. Siku moja baada ya Dk John Magufuli kuapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Marekani imeitaka Serikali yake kuutafutia ufumbuzi wa haraka mgogoro wa Zanzibar.

Katika tamko lake kuhusu Uchaguzi Mkuu, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry kupitia ubalozi wake hapa nchini jana, alisema taifa hilo linaendelea kushtushwa na tamko la mamlaka za Zanzibar kufuta matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25.

Oktoba 28, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha alitangaza kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu kwa madai ya kuwapo kwa kasoro mbalimbali na kwamba uchaguzi mwingine utafanyika baada ya miezi mitatu.

Tangu wakati huo, wanaharakati na watetezi wa masuala ya haki za binadamu kutoka ndani na nje ya visiwa hivyo wamekuwa wakiitaka Serikali ya Zanzibar kulitafutia ufumbuzi wa haraka suala hilo huku wengine wakiitaka ZEC kuendelea kutangaza matokeo.

“Kwa dhati kabisa, tunatoa wito kwa Serikali mpya kuhakikisha kuwa uamuzi wa watu wa Zanzibar unajidhihirisha katika ukamilishwaji wa haraka wa haki na wa amani wa mchakato wa uchaguzi visiwani Zanzibar,” alisema Kerry.Hii ni mara ya pili kwa Marekani kuzungumzia hatua ya ZEC kufuta matokeo hayo, awali taarifa ya ubalozi wa nchi hiyo jijini Dar es Salaam kwa vyombo vya habari ilisema kitendo kilichofanyika Zanzibar kinasitishia mchakato wa uchaguzi uliofanyika vizuri na kwa amani.

“Tunatoa wito wa kuondolewa kwa tamko hilo na kuzisihi pande zote kuhudhuria kwa dhati kuukamilisha mchakato huu wa kidemokrasia kwa uwazi na amani,” ilisema taarifa hiyo.

Pia, katika taarifa yake, Terry alimpongeza Rais Jakaya Kikwete na Watanzania kwa kufanikisha Uchaguzi Mkuu uliothibitisha rekodi nzuri ya Tanzania kuendelea kujenga demokrasia imara.“Wakati Rais Magufuli na Serikali yake wakichukua majukumu yao, tunatarajia kuendelea na ubia wetu wa karibu na kuimarisha zaidi ushirikiano baina ya nchi zetu mbili tunapofanya kazi pamoja ya kusaidia ujenzi wa demokrasia, kukuza usalama wa kikanda na kuendelea kuchochea maendeleo ya kiuchumi,” ilisema taarifa hiyo.

/Mwananchi.

No comments :

Post a Comment