Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, November 10, 2015

Mwinyi azindua kampuni ya vifaa vya ujenzi, kilimo


Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi
By Beatrice Moses, Mwananchi
Dar es Salaam. Rais Mstaafu  wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi amezindua kampuni kubwa ya China ya kuuza vifaa vya kilimo na ujenzi, ambapo ameeleza ni hatua kubwa katika safari ya maendeleo inayoshika kasi nchini.
Kampuni hiyo ya Avic-Shantui Tanzania Ltd, inatengeneza magari  ya ujenzi yakiwamo matingatinga, makatapila ya kushindilia na kusawazisha udongo na gari maalum la kuchanganya zege.
Akizungumza katika hafla ya uzunduzi wa kampuni hiyo uliofanyika leo jijini , Mzee Mwinyi amesema hatua ya uwekezaji huo mkubwa ni matunda ya urafiki wa baina ya nchi mbili ambazo ni China na Tanzania.
“ Ushirikiano wetu ni wa siku nyingi na umekuwa wa kidugu kwani China imekuwa ikitusaidia mambo mengi ikiwamo ujenzi wa reli ya Tazara, sasa hii kampuni inaanza kwa kuuza mitambo hiyo lakini wanatarajiwa kujenga kiwanda cha kuitengeneza hapa nchini mara mradi wa Mchuchuma na Liganga utakapokamilika,” amesema Mzee Mwinyi.
“ Wachina ni wakarimu kwetu, lakini ni wabunifu wazuri na wachapa kazi naamini siku zijazo tutashirikiana nao na kuzindua kiwanda cha kutengenezea mitambo hiyo hapa, ndipo Tanzania itakuwa makutano ya nchi nyingi kuja kununua zana za kilimo na ujenzi za kisasa,” amesisitiza.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Shantui Imp & Exp.co Chad Cheng amesema wanajivunia kuzindua kampuni hiyo nchini hapa wakishirikiana na kampuni ya Avic Intl  ambapo wanaongoza kwa uzalishaji wa mitambo na vifaa vya kilimo na ujenzi.
“ Tumejipanga katika kushiriki kuleta maendeleo ndani ya Afrika, tumewekeza katika nchi zaidi ya 30 bidhaa zetu zinatumika kwenye nchi zaidi ya 47, tunazalisha bidhaa bora na zenye viwango vya hali ya juu, tunaamini tutasaidia kukuza uchumi wa nchi kwa shughuli hizi,” amesema Cheng.

No comments :

Post a Comment