ZANZIBAR NI KWETU

Hili blog ni kuhusu Tanzania na dunia nzima kwa ujumla. Pita kila siku kwa habari moto moto.       (This blog is about Tanzania and the world as a whole. Pass-by everyday for breaking news). ***********************KARIBUNI NYOTE / YOU ARE ALL WELCOME!***********************

AirFreight

AirFreight

Kwarara Msikitini

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, November 29, 2015

Serikali yakanusha kuhusu hazina kuachwa tupu!


Serikali imekanusha taarifa zinazosambazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa amekomba fedha hazina na kuiacha Serikali bila fungu lolote.

Hayo yamesemwa jijini dare es salaam na Kamishina wa Bajeti kutoka Wizara ya Fedha Bwa. John Cheyo huku akiwataka wananchi kupuuza habari hiyo kwani hazina ukweli wowote.

Hazina inazo pesa za kutosha na tunajivunia kufanya uchaguzi wa mwaka huu, kununua mashine za BVR kwa kutumia pesa za watanzania bila kutegemea msaada wowote kutoka nje ya nchi na kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu mwaka huu? alisema Bwa. Cheyo.

Pia aliongeza kuwa serikali imeendelea kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa bomba la gesi ambalo limekamilika hivi karibuni, vinu vya kuchakata gesi na ujenzi wa barabara nchini.

Aliendelea kusema kwamba mfumo wa serikali wa bajeti unaiwezesha serikali kupanga vipaumbele vya matumizi kulingana na bajeti ilivyopangwa ambapo fedha zinazokusanywa kupitia mfuko mkuu wa serikali ndizo hutumika.

Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge kwa kipindi cha 2015-2016 ni shilingi Trilioni 22.5 na bajeti hiyo inatengenezewa mpango wa makusanyo na matumizi kwa kulipia mishahara ya wafanyakazi na miradi mbalimbali iliyoidhinishwa.

Pia katika matumizi mengine bajeti hiyo inalipia chakula cha wanafunzi, mikopo ya wanafunzi elimu ya juu, ununuzi wa dawa na vifaa tiba na chakula cha hifadhi ya taifa.

http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/978880-serikali-yakanusha-kuhusu-hazina-kuachwa-tupu.html 

at 9:20 AM
Email This BlogThis! Share to X Share to Facebook Share to Pinterest

No comments :

Post a Comment

Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments ( Atom )

Search This Blog

Click here to advertise with us!
Tweets by @znzkwetu

Books On Zanzibar Isles

Popular Posts

  • UAE's 47 billionaires control Dh598b wealth, says report! UAE's 47 billionaires control Dh598b wealth, says report!
  • Now perform Umrah throughout the year! Now perform Umrah throughout the year!
  • no image Vodacom launches 947m/- promotion
  • سورة الكهف كاملة (مكتوبة ) للقارئ الشيخ محمد الفقيه _ تلاوة خاشعة ومؤثرة😌💚 سورة الكهف كاملة (مكتوبة ) للقارئ الشيخ محمد الفقيه _ تلاوة خاشعة ومؤثرة😌💚
  •  Uganda’s Oil Journey: From Discovery to a Seat at the Global Decision-Making Table! Uganda’s Oil Journey: From Discovery to a Seat at the Global Decision-Making Table!

Pages

  • Contact us
  • Zanzibar Ni Kwetu Online Store
  • ZSSF PROJECT AT MBWENI, ZANZIBAR.
  • Advertise with zanzibar ni kwetu
  • MADUKA MAPYA YANAKODISHWA MWANAKWEREKWE, ZANZIBAR MKABALA NA MARIKITI!!!
online
Follow @znzkwetu

KITETE BEACH BUNGALOWS!

KITETE BEACH BUNGALOWS!

Shops for rent at Mwanakwerekwe, Znz

Shops for rent at Mwanakwerekwe, Znz

Shops for rent at Fuoni, Zanzibar!

Shops for rent at Fuoni, Zanzibar!

Zanzibar-Canadian Diaspora Association

Zanzibar-Canadian Diaspora Association
*************ZACADIA*************

****Zanzibar - Canadian Association****

****Zanzibar - Canadian Association****
*************ZANCANA*************

****Join the Zanzibar Ni Kwetu Team****

****Join the Zanzibar Ni Kwetu Team****

***The People's Bank of Zanzibar Ltd***

***The People's Bank of Zanzibar Ltd***
SEND MONEY FROM THE COMFORT OF YOUR HOME TO TANZANIA @ LOW FEES!

Zanzibar Properties

Zanzibar Properties

Visitors

Sparkline

Blog Archive

Copyright 2025. Zanzibar Ni Kwetu Blog. All Rights Reserved.. Powered by Blogger.