Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, November 4, 2015

TB Joshua ateta na Magufuli, Lowassa

Rais Jakaya Kikwete, akizungumza na Nabii Temitope Balogun Joshua Ikulu jijini Dar es Salaam jana. TB Joshua amekuja nchini kuhudhuria kuapishwa kwa Rais Mteule, Dk. John Magufuli.
Ujio wa Nabii wa Kimataifa kutoka Nigeria, TB Joshua aliyetua jijini  Dar es Salaam jana na kupokewa na Rais mteule wa awamu ya tano, Dk.  John Magufuli na baadaye kwenda kwa aliyekuwa mgombea urais wa  Chadema, Edward Lowassa, umeibua gumzo kubwa kuhusiana na matokeo ya  uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25.
 
Nabii huyo wa Kanisa la The Synagogue, Church of All Nations (SCOAN),  aliwasili nchini jana jioni kushuhudia kuapishwa kwa Magufuli kesho.
 
Wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti jana ikiwa ni muda mfupi  baada ya taarifa za kuwasili nchini kwa TB Joshua kusambaa kupitia  mitandao mbalimbali ya kijamii, baadhi ya wananchi walisema ujio wa  Nabii huyo aliyepokewa na Magufuli ikiwa ni siku mbili tu kabla ya  kuapishwa kwa Rais huyo mteule ni ishara kuwa kweli, kuna siku  aliwahi kumtabiria ushindi kabla ya kuanza kwa kinyang’anyiro cha  kuwania urais.
 
Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina moja la Aggrey,  mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam, aliiambia Nipashe kuwa hapo  kabla, aliwahi kusikia Dk. Magufuli ni miongoni mwa wanasiasa  waliowahi kutabiriwa mambo mazuri na TB Joshua na hivyo, ujio wake  huo ikiwa ni muda mfupi kabla ya kuapishwa kwake unampa imani kwamba  aliyokuwa akiyasikia ni ya kweli tupu.“Yawezekana wana urafiki mkubwa baina yao… inawezekana ni kweli  aliwahi kumtabiria ushindi huu alioupata. Hata hivyo, vyovyote  itakavyokuwa sawa tu kwa sababu TB Joshua ni kiongozi mkubwa wa  kidini na Magufuli ndiye kiongozi wetu wa awamu ya tano. Muhimu ni  kwa Nabii huyu amuombee Magufuli kutimiza yale aliyotuahidi  Watanzania wakati wa kampeni za uchaguzi,” alisema mkazi huyo wa  Sinza.
 
Mkazi wa Kigogo Luhanga jijini Dar es Salaam, Salum Mahwata, alisema  ni jambo zuri Magufuli kuonekana akiwa karibu na TB Joshua kwani  yawezekana hiyo ni dalili kuwa ataendeleza desturi ya kuheshimu  viongozi wa kiroho na kufanyia kazi ushauri watakaokuwa wakiutoa  kwake kwa maslahi ya taifa. “Labda jambo kubwa la kuzingatia ni kuona  kuwa Magufuli atatoa nafasi kwa viongozi wengine pia wa kidini  wakiwamo wa hapa nyumbani na tena wa madhehebu mengine ili kuonyesha  kuwa wote anawahitaji katika kuliendeleza taifa letu… hili ni jambo  zuri,” alisema Mahwata.
 
Wengine waliowahi kutabiriwa ni Lowassa, ambaye katika picha  zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii mwaka huu, zilionyesha akiwa  katika ibada katika kanisa la Nabii huyo.
 
Kadhalika, gumzo zaidi kuhusiana na ujio huo wa TB Joshua  liliongezeka zaidi jioni baada ya picha nyingine kusambazwa kwenye  mitandao zikimuonyesha akiwa na aliyekuwa mgombea urais wa Chama cha  Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, ambaye pia alikuwa  akiwakilisha Muungano wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya  Wananchi (Ukawa).
 
Msemaji wa Lowassa, Abubakar Liongo, jana alithibitisha ujio wa TB  Joshua kwa Lowassa, alipoongea na Nipashe kwa njia ya simu.
Kama ilivyokuwa kwa taarifa za kuwa na Magufuli, taarifa na picha  hizo za TB Joshua na Lowassa pia ziliibua mijadala mbalimbali kwenye  mitandao ya kijamii.
 
Baadhi ya watu waliokuwa wakichangia mijadala hiyo kuhusiana na ujio  wa TB Joshua walidai kuwa ni jambo zuri kwani amekuja kusaidia maombi  ya kudumisha amani nchini baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu.
 
Magufuli anatarajiwa kuapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania kesho baada ya kuibuka na ushindi wa asilimia zaidi ya  58.46, akifuatiwa na Lowassa aliyepata asilimia 39.97
 
UJIO WAKE
Taarifa na picha zilizosambazwa awali jana zilionyesha kuwa Nabii  Joshua alipokewa kwenye Uwanja wa Ndege jijini Dar es Salaam na  mwenyeji wake, Rais Mteule, Dk. Magufuli jana jioni.
Ilieleza kuwa mara baada ya kuwasili, TB Joshua alikwenda moja kwa  moja Ikulu na huko alikutana na Rais Jakaya Kikwete anayekaribia  kumaliza muda wake.
 
Inaelezwa kuwa katika salamu zake, TB Joshua alimpongeza Rais Kikwete  kwa kufanikisha uchaguzi mkuu uliofanyika kwa uhuru na amani, huku  akiondoka madarakani akiwa mtu mwenye furaha.
 
“TB Joshua alimpongeza Kikwete kwa kumpata Dk. Magufuli kama mrithi  wake, akimtaja rais huyo mpya mteule kama Rais wa Tanzania wa baraka  na fanaka tele katika awamu hii mpya,” ilisema sehemu ya taarifa  iliyoripotiwa jana.
 
Kadhalika, taarifa hiyo iliambatana na picha zinazomuonyesha TB  Joshua akisalimiana na Rais Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaama.
Ilielezwa zaidi kuwa TB Joshua aliwasili nchini na watu 40 ambao wote  watashuhudia kuapishwa kwa Dk. Magufuli kesho.
 
Baadhi ya picha zilimuonyesha Dk. Magufuli akiwa na mkewe, Janeth  Magufuli, wakimpokea TB Joshua kwenye uwanja wa ndege na nyingine  wakiwa nyumbani kwake (Magufuli).
 
UTABIRI WA TB JOSHUA
Miezi michache kabla ya kuanza kwa mchakato wa kumsaka mgombea urais  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na hasa baada ya Dk. Magufuli kuchukua  fomu ya kuomba ridhaa ya chama hicho kugombea urais, picha zilisambaa  kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha yeye (Magufuli), mkewe  (Janeth Magufuli) na mtoto wao mmoja wa kiume wakiwa kwa Nabii huyo.
 
Wakati huo, ilielezwa kuwa TB Joshua alimtabiria Dk. Magufuli kuwa  siku moja atakuwa Rais wa Tanzania. Hata hivyo, taarifa hizo  hazikuthibitishwa wakati huo, kwani wengine waliowahi kuonekana  wakiwa kwa TB Joshua ni pamoja na mgombea urais wa Chama cha  Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aliyewakilisha pia Umoja wa Katiba  ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa na pia mtia nia mwingine kati ya  38 wa CCM, Mwigulu Nchemba.
 
Kanisa la TB Joshua la Scoan huendesha kituo cha luninga cha  Emmannuel TV, ambacho kimejitwalia umaarufu mkubwa.
 
TB Joshua amewahi kutunukiwa nishani kama ‘Officer of the Order of  the Federal Republic’ (OFR) na serikali ya Nigeria mwaka 2008 na pia  aliwahi kuchaguliwa kuwa mtu wa Karne toka kabila la Yoruba nchini  Nigeria. Alipewa wadhifa huo na taasisi ijulikanayo kama Pan-Yoruba  media outlet Irohin-Odua.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment