Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, November 4, 2015

TB Joshua, marais wanane Afrika kushuhudia kuapishwa Magufuli!

Aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa akisalimiana na TB Joshua, wakati akimkaribisha nyumbani kwake, Masaki, Dar es Salaam jana. Picha na Othman Michuzi
By Peter Elias, Mwananchi
Dar es Salaam. Marais wanane wa Afrika wamethibitisha kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais mteule, Dk John Magufuli itakayofanyika kesho katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Pia, sherehe hizo zitahudhuriwa na nabii TB Joshua wa Kanisa la Synagogue Church of All Nations (Scoan) kutoka Nigeria ambaye aliwasili nchini jana na kukutana na Rais Jakaya Kikwete Ikulu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, marais watakaohudhuria shughuli ya kuapishwa kwa Dk Magufuli ni Robert Mugabe (Zimbabwe), Yoweri Museveni (Uganda), Paul Kagame (Rwanda), Jacob Zuma (Afrika Kusini), Joseph Kabila (DRC), Uhuru Kenyatta (Kenya), Filipe Nyusi (Msumbiji) na Edgar Lungu (Zambia).
Malawi itawakilishwa na Makamu wa Rais, Saulos Chilima wakati Namibia ikiwakilishwa na Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Netumbo Nandi-Ndaitwah.
China itawakilishwa na Makamu Mwenyekiti wa chama tawala cha CPC. Nchi nyingine ambazo zimethibitisha kushiriki na ambazo zitawakilishwa na kati ya makamu wa rais, waziri mkuu, spika au balozi ni Burundi, Comoro, Angola, Botswana, Lesotho, Madagascar na Mauritius.
Taarifa hiyo ilitaja nchi nyingine zitakazotuma wawakilishi kuwa ni Norway, Oman, Sudan Kusini, Sweden, Umoja wa Falme za Kiarabu, Marekani, Uingereza, Shelisheli, Swaziland, Algeria, Misri, Benin, Denmark, Ethiopia, Finland, Ufaransa, Ghana, India, Japan, Kuwait, Uholanzi na Nigeria. Wakuu wa mashirika ya kimataifa na kikanda waliothibitisha kushiriki au kutuma wawakilishi wao ni pamoja na Umoja wa Mataifa (UN), Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Umoja wa Ulaya (EU), Jumuiya ya Ukanda wa Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR).

No comments :

Post a Comment