Baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kupoteza baadhi ya majimbo ya uchaguzi katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini, Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa chama hicho, wilaya ya Moshi (UVCCM), kimeitaka serikali kuangalia uwezekano wa kuandaa muswada wa marekebisho ya sheria ya uchaguzi.
Jumuiya hiyo inadai kuwa, kama ushauri wao utathaminiwa na kutekelezwa, sheria ya uchaguzi itakayofanyiwa marekebisho, itasaidia kuwabana wasimamizi wa uchaguzi watakaobainika kuhujumu zoezi la uchaguzi na utangazaji wa matokeo.
Katibu wa Jumuiya hiyo, Joel Makwaiya alisema serikali ya awamu ya tano ina kila sababu ya kufanya tathimini ya jumla ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu na kuandaa muswada utakaofanyiwa marekebisho ili uwe na kipengele kitakachowabana wasimamizi wa uchaguzi watakaovurunda.
Makwaiya alikuwa akizungumza jana wakati wa kikao cha maazimio ya Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM, kilichoketi kupitia mchakato wa upigaji kura, kuhesabu kura na utangazaji wa matokeo ya ubunge na udiwani.
“Lakini pia tumekishauri chama (CCM) ngazi ya wilaya kufungua kesi mahakama kuu ya Tanzania, kanda ya Moshi, kupinga matokeo ya ubunge yaliyompa ushindi mbunge mteule wa jimbo la Moshi Mjini (Chadema), Japhary Michael," alisema.
Madai hayo yamekuja wakati ambapo aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM, Davis Mosha, akiwa ametangaza rasmi kuachana na siasa, akidai kwamba chama chake kimejaa wanafiki, jambo lililochangia kuanguka kwake.
Katika uchaguzi huo, Meya wa zamani wa jimbo hilo, Michael alishinda kiti cha ubunge.
Wengine walioshiriki uchaguzi huo ni wagombea ubunge na vyama vyao kwenye mabano, Buni Ramole (ACT-Wazalendo), Isaac Kireti (Sau) na Godlisten Kitali (UDP). Katikajimbo hilo Chadema imeshinda viti 19 vya udiwani na CCM imeambulia viti viwili kati ya kata 21 zilizopo Moshi Mjini.
Alisema UVCCM imepitia kwa kina mchakato mzima wa uchaguzi huo na kubaini kwamba kulijitokeza dosari mbalimbali ambazo zimeacha mashaka kuwa uchaguzi huo haukuwa huru na wa haki.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments :
Post a Comment