Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 13, 2015

Balozi Seif asitisha ujenzi wa nyumba ya ghorofa mtaa wa Mlandege

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwasili mtaa wa Mlandege  kukagua kiwanja cha nyumba ya Ghorofa kinacholalamikiwa na Wakaazi wa Mtaa huo kwamba kimevamia pia eneo la wazi linalotumika kwa shughuli za Kijamii.
  Balozi Seif akipokea malalamiko ya Wakaazi wa Mtaa wa Mlandege wakimshutumu Mmiliki wa Kiwanja cha jengo la Ghorofa Bwana  Anuari Abdulla anayejenga pamoja na eneo la wazi.
 Mmiliki wa Kiwanja cha nyumba ya Ghorofa Mlandege Bwana Anuari Abdullah akijitetea kupata kibali kinachomruhusu kuendeleza ujenzi wa nyumba yake.

Baadhi ya Wakaazi wa Mtaa wa Mlandege wakitafakari na kufurahia maamuzi yaliyochukuliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ya kuzuia ujenzi wa jengo la Ghorofa kwa kukosa taratibu zinazozingatia Mji mkongwe wa Zanzibar.

Picha na – OMPR –ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amemuagiza Mmiliki wa Kiwanja kinachotaka kujengwa Nyumba ya Ghorofa katika Mtaa wa Mlandege Bwana Anuari Abdulla kusitisha mara moja ujenzi huo.

Hatua hiyo ya Balozi Seif imekuja kufuatia malalamiko makubwa yaliyotolewa na wakaazi wa Mtaa huo wakimshutumu Mmiliki huyo kuvamia pia eneo la wazi        { Open Space } la shughuli za kijamii katika sehemu hiyo.

Balozi Seif alimuonya Mmiliki huyo kwamba endapo ataendelea kukaidi agizo alilopewa na Mamlaka Nne zinazosimamia na kushughulikia masuala ya Ujenzi  Serikali italazimika kumchulia hatua za kisheria dhidi yake.“ Tumebaini kwamba unaendelea kwenda kinyume na maamuzi uliyopewa ya kusitisha ujenzi wa Jengo lako. Sasa endapo utaendelea kufanya hivyo Serikali italazimika kukuchukulia hatua za kisheria zinazofaa “. Alisema Balozi Seif.

Alifahamisha kwamba wakaazi wa Mtaa wa Mlandege ambao wanaishi ndani ya eneo la Mji Mkongwe lililopata hadhi ya kuwa Urithi wa Kimataifa wanapaswa kuzingatia matakwa yaliyokubalika katika uhifadhi wa Mji huo wa Kihistoria.

Mapema Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji Mji Mkongwe wa Zanzibar Nd. Issa Sarboko Makarani alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Mmiliki wa kiwanja hicho amekuwa akikaidi maamuzi anayopewa kuyatekeleza na mamlaka husika katika ujenzi huo.

Nd. Sarboko alisema Bwana Anuari ameamua kuendeleza ujenzi huo kwa kutumia kibali alichopewa na Mmoja wa Afisa wa Baraza la Manispaa ambacho tayari kimeshafutwa kwa vile kinakiuka  na kutozingatia sheria na taratibu zilizowekwa.

Alisisitiza kwamba Mmiliki huyo tayari ameshaonywa na Viongozi wa Taasisi Nne waliokutana kujadili suala hilo na kumtaka asubiri maamuzi ya pamoja yatakayotolewa baada ya kuzingatia hali halisi ya namna yatakavyozingatia matakwa na haki ya kila upande unaohusika.

“ Kibali cha Ujenzi wa Jengo hili kinachodaiwa kutolewa na Baraza la Manispaa Zanzibar kimefutwa kwa pamoja na wakurugenzi Wanne wa Idara za Ardhi, Mamlaka ya Mji Mkongwe, Baraza la Manispaa pamoja na Idara ya Ujenzi na Mipango Miji “. Alifafanua Nd. Sarboko.

Alimtaka Mmiliki huyo kuhakikisha kwamba mabati yaliyowekwa kufunga eneo la wazi lililokuwa likitumika kwa wapita njia pamoja na kutumika kwa shughuli za Kijamii anayaondoa mara moja vyenginevyo watendaji wa Mamlaka hiyo watalazimika kutekeleza amri hiyo kwa kutumia kijiko katika kipindi kifupi kijacho.

No comments :

Post a Comment