Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 20, 2015

CDA yavunja nyumba 180 zilizojengwa kiholela

Kizota resident in Dodoma Region falls down in shock after her house was demolished by Capital Development Authority (CDA) in Dodoma yesterday for allegedly building at the non-sanctioned area. (Photo: Correspondent Ibrahim Joseph)

Jumla ya Nyumba na mapagale 180 yamevunjwa na Mamlaka ya ustawishaji Makao Makuu (CDA), kutokana na uvamizi na  kujenga bila kufuata sheria za mipango miji.


Akizungumza na NIPASHE, Afisa Uhusiano wa mamlaka hiyo, Angela Msimbila, alisema lengo la kubomoa nyumba hizo ni kuwataka wananchi wajenge kwa kufuata taratibu.

Alisema watu hao wamebomolewa kutokana na kujenga kwenye maeneo ya watu wengine ambao wana vibali halali.

"Tumebomoa Dachi B Centre nyumba na mapagale 177 lakini nyumba 27 ndizo zilikuwa na watu ndani, pia kulikuwa na hayo mapagale ambayo yalikuwa yametegeshwa ambayo ni ya nyumba za udongo, na nyumba moja tu ndio ilikuwa ya matofari ya saruji," alisema Msimbila

Aliongeza wamefikia hatua hiyo kutokana na wamiliki halali wa maeneo hayo kutishiwa maisha na wavamizi katika maeneo hayo.

"Kuna watu ambao walikuwa na barua ambazo zinawatambulisha kuwa wao ni wamiliki halali wa viwanja, lakini wanashindwa kuviendeleza viwanja vyao kutokana na wavamizi kuvamia maeneo yao," alibainisha Msimbila

Alitaja maeneo mengine kuwa ni Chinangali ambapo ilivunjwa nyumba moja ambayo ilijenga maduka matatu na uzio bila kufuata taratibu za mipango miji na pia Bahiroad ilivunjwa nyumba moja ambayo pia ilijengwa bila kufuata ramani aliyopewa.

Alitoa wito kwa wananchi kufuata ramani za ujenzi wanazopewa badala ya kujiongezea na wengine kujenga kitu ambacho hakitakiwi kujengwa kwenye eneo hilo.

Msimbila alisema zoezi hilo litakuwa endelevu katika maeneo yote ili wananchi wafuate taratibu na sheria huku akisema wametoa notisi kwa watu wote ili waweze kuondoka katika maeneo hayo.

Polisi wasimamia zoezi.
Zoezi hilo limeendeshwa na mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ambapo wananchi wamelalamikia hatua hiyo na kudai kuwa hawakupewa muda ili waweze kuondoka.

Vilio vyatawala
Wananchi waliokumbwa na mkasa huo waliangua vilio kutokana na kubomolewa nyumba zao.
Akizungumzia hali hiyo, Mmoja wa wananchi hao, Mwajuma Hamis, alisema zoezi hilo limekuwa la kushtukiza na hawaelewi mpaka sasa wataenda wapi na limewarudisha nyumba kimaendeleo.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment