Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 13, 2015

Dk Shein, Aizundua Meli Mpya ya MV Mapinduzi II Zanzibar.

Meli Mpya ya MV MAPINDUZI ikiwa imefunga Gati ya Malindi wakati wa Uzinduzi wake uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwasili katika bandari ya Zanzibar akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe Abdalla Mwinyi Khamis.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwasili katika bandari ya Zanzibar akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwasili katika bandari ya Zanzibar akisalimiana na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, alipowasili katika eneo la bandari ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Abdalla Juma,akitowa maelezo kwa Rais sehemu ya kukaa abiria wakisubiri kupanda katika Meli ikiwa katika eneo la Bandari ya Malindi Zanzibar 
Sehemu ya kupumzikia abiria wakisubiri kupanda Meli iliojengwa na Shirika la Bandari Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akiwa na Mkurugenzi wa Bandari na Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano, wakitembea kuelekea sehemu ya Gati ya Malindi kwa ajili ya uzinduzi wa Meli Mpya ya Mv Mapinduzi 2.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Afisa Uhusiano wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Nafisa Madai akitowa maelezo kwa Rais Dk Shein, kuhusiana na utengenezaji wa Meli hiyo wakati wakitiza TV. ikionesha jinsi ya utengenezaji wa Meli hiyo huko Nchini Korea ya Kusini. 













Sehemu ya VIP ina uwezo wa kuchukua abiri 55.
       Waheshimia wakiwa katika sehemu ya daraja la kwanza 
Mfanyakazi wa Meli ya Malipinduzi  II akiwa katika sehemu ya abiria daraja la kwanza 
Sehemu ya mgahawa kila sehemu ya abiria inajitegemea kwa mgahawa wake kwa kutoa huduma ya chakula kwa abiria
Sehemu ya kukaa Abiria wa daraja la Pili 
Sehemu ya maegesho ya magari yanayopakiwa kusafirishwa ina uwezo wa kuchukua magari 60
Chumba cha kuhifadhia maiti kikiwa katika meli hiyo na Kuna sehemu ya msikiti kwa ajili ya kusalia Abiria wakiwa safarini. 
Moja ya Boti za Kuokolea ikitokea Dharuwa wakati safari zake ikiwa na uwezo wa kuchukua abiria 66 kwa wakati mmoja 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akiteremka katika Meli ya Mv Mapinduzi  II baada ya kuizindua na kuitembelea Meli hiyo ya Mpya na ya Kisasa kujionea vitu mbalimbali vilioko katika Meli hiyo. 
/ZanziNews.

Dk Shein apongeza kamati iliyosimamia utengenezaji meli ya MV Mapinduzi II

Na Khadija Khamis –Maelezo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti  wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein ameipongeza kamati ya usimamizi  iliyoshughulikia utengenezaji wa Meli Mpya Mapinduzi II kwa kuweza kukamilika kwake.

Pongezi hizo alizitoa leo huko Bandarini wakati wa uzinduzi wa Meli hiyo ya kisasa ya ambayo imetengenezwa na Kampuni ya Daewoo International  kutoka  Korea ya Kusini.

Alisema kuwa Meli hiyo ni mpya na yenye mitambo ya kisasa yenye uwezo mkubwa  ambayo haiyumbishwi, kwani ina vyombo maalumu vya kurekebisha mwenendo wa mawimbi mkondoni.

“Wananchi Msisikilize maneno ya mitaani kuwa Meli imeshatumika suala hilo halina ukweli, nawataka muje kuitembelea meli hiyo ili  kuweza kujionea wenyewe”. Amesema Dkt Shein.

Aidha alisema kuwa utaratibu wote wa utengenezaji tokea hatua ya awali hadi kumalizika kwake umeonyesha na Kampuni ya Daewoo ya Korea haiwezi kudanganya na kuihadaa Dunia na imeweza kugharimu Dola million 30.4 za kimarekani na ujenzi ulianza mnamo July 2013 hadi Disemba 2015 kuwasili Zanzibar.

Rais wa Zanzibar alisema kuwa kazi iliokuwepo  hivi sasa ni wananchi kuweza kuitunza  na kuihifadhi  meli hiyo ibakie kuwa na haiba na uzuri wake.

Aidha alisema kuwa Meli ya Mapinduzi II ni mpya na ya kisasa  yenye uwezo mkubwa wa kusafirisha abiria 1200  na mizigo tani 200.

Alifahamisha kuwa kukamilika kwa meli hii mabadiliko makubwa yameweza kufanyika katika shirika la meli na uwakala tiketi zinauzwa kwa njia za kutumia komputa abiria hawezi kuuziwa tiket mpaka awe na kitambulisho cha Mzanzibar ,Mtanzania au kwa mgeni awe shahada ya kusafiria.

Pia alieleza kuwa Serikali inategemea kuweka Bandari kubwa ya mizigo eneo la Maruhubi mpiga duri na tayari imeshaanza makubaliano na Serikali ya China kuanzia mwezi wa Januari au Febuari wanatarajiwa kuanza  kazi ya ujenzi.

Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Utengenezaji wa Meli ambae pia ni Waziri wa Fedha Omar Yusuf Mzee amesema ameridhika na umalizaji wa meli hiyo na kutoa shukrani kwa wale wote waliokuwa sambamba katika kukamilisha kazi hiyo.

No comments :

Post a Comment