Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, December 13, 2015

Fagia fagia ndani ya CCM yaja

Kasi ya Rais John Magufuli ya kutumbua majipu serikalini inatarajiwa kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM), mara tu atakapokabidhiwa rungu la Uenyekiti na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.


Mara tu atakapokabidhiwa rungu la uenyekiti, Magufuli anatarajiwa kufanya kile anachoendelea kukifanya ndani ya serikali kwa kuwaumbua viongozi ndani ya chama hicho waliojigeuza miungu watu na wanaoharibu taswira ya chama.

Habari kutoka ndani ya CCM zinasema kuna viongozi ambao wamejimilikisha na wamekuwa wakineemeka kwa miradi mbalimbali ya chama hicho huku kikitegemea ruzuku ya serikali kujiendesha.

Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, aliandika katika ukurasa wake wa Twitter wiki iliyopita kwamba baada ya kumaliza serikalini, mabadiliko yatahamia hapo, Nnauye ameapishwa jana kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo.

Mmoja wa viongozi wandamizi ndani ya CCM, aliliambia gazeti hili kwamba Magufuli anatarajia kutembeza fagio la chuma atakapokabidhiwa uenyekiti ili kurudisha heshima ya chama hicho kwa jamii.

Kiongozi huyo ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini, alisema hivi sasa wafanyabiashara wengi na matajiri wamekimbilia CCM na wengine kutumia mamilioni ya fedha kutafuta vyeo ikiwa ni ujanja ujanja wa kuficha maovu yao.

“Hivi sasa kama huna fedha usijisumbue kugombea nafasi ndani ya chama maana hutapata kitu, chama ni kama kimegeuka cha matajiri (na) maskini hawana chao tena,” alisema.

“(Lakini) sasa Magufuli hatapenda kuona hali hii ikiendelea. Kuna watu lazima watakwenda na maji. “Imefikia wakati watu wenye tuhuma mbalimbali za ufisadi na wengine wakituhumiwa kwa kufadhili vikundi vya ujambazi wanawania kuteuliwa na chama kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama.

“Ndiyo maana wananchi wakakichoka chama sasa, Rais Magufuli kwenye kampeni zake za urais alibaini hilo na lazima atembeze fagio la chuma.”
Mbunge wa Chunya (CCM), Victor Mwambalaswa, alisema  ni kweli chama kimevamiwa na watu ambao hawana sifa ya kuwa kwenye chama hicho.

Alisema wanachama hao ndio wanaofanya CCM kuchukiwa na wananchi kwa kuonekana kama chama cha mafisadi wakati kimefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

ìKama kuna mfanyabiashara anataka kuingia katika siasa aingie lakini asiifanye CCM kama kichaka cha kuficha maovu yake, ukiwa mwanasisasa kuwa mwanasiasa na ukiwa mfanyabiashara basi kuwa mfanyabaishara,î alisema Mwambalaswa.

Alisema endapo Rais Magufuli atakisafisha chama, basi wenye nia mbaya na CCM watakuwa wa kwanza kuondoka.

Naye Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy Mohamed, alisema ndani ya CCM siyo wafanyabiashara tu wanaoenda kinyume na katiba ya chama bali kuna hata wabunge ambao wanakifanya chama kama mwamvuli wa kupitisha mambo yao.

“Kuna watumishi wa serikali, wabunge, na wafanyabishara ambao wako ndani ya chama na wanafaidika kupitia mgongo wa chama, ila nina imani tumepata Rais ambaye atakisafisha chama na kitakuwa safi.” alisema Keissy.

Imekuwa kawaida kwa Mwenyekiti wa CCM kumwachia nafasi hiyo Rais aliyeko madarakani hata kabla ya muda wa uchaguzi ndani ya chama kufika.

CCM inatakiwa kufanya uchaguzi mkuu 2017 lakini wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaona Kikwete atamkabidhi nafasi ya uenyekiti Rais Magufuli mwakani.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment