Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Donan Mmbando, aliyasema hayo alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Mmbando aliitaja mikoa itakayopewa dawa hizo za Ivermectin na Albendazole kwa ajili ya matende na mabusha kuwa ni Dar es Salaam, Katavi, Rukwa, Singida, Dodoma, Mtwara, Lindi na Pwani “Mikoa mingine iliyobaki mpango huo wa ugawaji wa dawa ngazi ya jamii na shuleni, utafanyika mwishoni mwa Januari hadi Februari, mwakani,” alisema.
Hata hivyo, alisema watoto wenye umri wa miaka mitano, wajawazito, wanaonyonyesha chini ya siku saba na wagonjwa mahututi, hawa yapewa dawa hizo.
Aidha, katika udhibiti, ukomboaji na usambazaji wa dawa, serikali imetoa Sh. milioni 500 kuhakikisha kwamba magonjwa hayo yanatokomezwa ifikapo mwaka 2020.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment