Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, December 18, 2015

Wagombea urais Z'bar wataka warejeshewe gharama zao

Mwenyekiti wa Zec, Jecha Salim Jecha
Baadhi ya wagombea urais wa Zanzibar, wamecharuka wakitaka warejeshewe fedha za gharama za kampeni na dhamana ya kugombea nafasi hiyo kama Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) imeshindwa kukamilisha Uchaguzi Mkuu.
 
Walitoa msimamo huo walipokuwa wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti mjini hapa jana kuhusiana na kutofanyika kwa uchaguzi huo tangu Mwenyekiti wa Zec, Jecha Salim Jecha, afute Oktoba 28, mwaka huu.
 
Mgombea wa urais wa Zanzibar, Juma Ali Khatib (Tadea), alisema tangu kufutwa matokeo, wamebaki njia panda kutokana na Zec kushindwa kuwafahamisha kinachoendelea.
 
Kwa mujibu wa Khatib, gharama zake za kuwania nafasi hiyo zikiwamo za kampeni Sh. milioni 70 na fedha za dhamana Sh. milioni mbili.
 
Mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya AFP, Soud Said Soud, alisema mazungumzo yanayoendelea kufanywa kuhusu mgogoro wa kisiasa Zanzibar, yamepora mamlaka ya Zec kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.“Zec ichukue mamlaka yake, mazungumzo ya viongozi wa Kitaifa na Marais wastaafu, hawana mamlaka ya kusimamia au kuamua matatizo ya uchaguzi zaidi ya Tume yenyewe,” alisema Soud.
 
Alisema wagombea wa urais Zanzibar, hawakupaswa kutengwa katika meza ya mazungumzo kwa sababu wote walikuwa na sifa na haki sawa kabla ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu.
 
Alisema kama Zec imeshindwa kukamilisha uchaguzi mkuu, irejeshe gharama za kampeni na dhamana za wagombea Sh. milioni mbili kila mgombea wa nafasi ya urais.
 
Mgombea wa Jahazi Asilia, Kassim Bakary Ali, alisema baada ya kufutwa matokeo ya uchaguzi mkuu, walitarajia Zec ingewaita na kuwafahamisha, lakini iko kimya licha ya kutumia gharama kubwa katika uchaguzi huo.
 
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Uchaguzi Mipango na Uchaguzi wa Chama cha Wananchi (CUF), Omar Ali Shehe, alisema hakuna tatizo kwa vyama vingine kutengwa katika mazungumzo ya suluhu ya mgogoro wa kisiasa Zanzibar.
Juhudi za kumpata Mwenyekiti wa Zec na Katibu Mkuu Kiongozi, kuzungumzia malalamiko hayo hazifanikiwa jana.

CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment