Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, December 11, 2015

Sura mpya 17 ndani baraza la JPM

Rais John Magufuli akifurahia jambo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue baada ya kutangaza Baraza la Mawaziri Ikulu jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Picha na Ikulu
By Suzan Mwillo, Mwananchi
Dar es Salaam. Miongoni mwa mawaziri na manaibu waziri walioteuliwa kwenye baraza jipya la   Rais John Magufuli, zimo sura mpya 17 ambazo zimeteuliwa kwa mara ya kwanza.
Sura mpya hizo za mawaziri katika baraza hilo ambalo uteuzi wake umechukua muda mrefu ni Nape Nnauye ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo.
Nape ambaye alishinda ubunge katika jimbo la Mtama katika Uchaguzi Mkuu kwa mwaka  huu ameteuliwa kuwa waziri kwa mara ya kwanza katika Serikali ya awamu ya tano.
Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi wa CCM,  ataitumukia wizara hiyo pamoja na naibu wake Anastazia Wambura ambaye pia ni mbunge wa viti maalumu wanawake wa  chama hicho.
Naibu Waziri aliyeteuliwa kusimamia Wizara ya Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala bora ni Jafo Seleiman Said ambaye pia ni mbunge wa Kisarawe.
Katika Wizara ya Ofisi ya Makamo wa Rais inayoshughulikia Muungano na Mazingira, Rais Magufuli amemteua  Luhaga Mpina kuwa naibu waziri wa wizara hiyo.
Mpina amekuwa mbunge wa Jimbo la Kisesa tangu mwaka 2005.
Chini ya Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Rais Magufuli ameteua manaibu waziri wawili kusimamia  wizara hiyo.
Manaibu hao ni Mwalimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Dk Possy Abdallah ambaye pia  ameteuliwa kuwa mbunge, mwingine ni  Anthony Mavunde, mbunge wa Dodoma Mjini.
Hata hivyo, Mei mwaka huu Rais mstaafu Jakaya Kikwete alimteua Mavunde kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa.
Katika Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi naibu waziri atakayesimamia ni mbunge wa Ngorongoro  William Ole Nasha huku Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano naibu wake ni Mhandisi Edwin Ngonyani.
Rais Magufuli amemteua Dk Ashantu Kizachi kuwa naibu waziri wa Wizara ya Fedha na Mipango na Dk Medard Karemaligo kuwa naibu waziri wa Nishati na Madini.
Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa, aliyeingia kwenye ulingo huo kwa mara ya kwanza ni Dk Augustine Mahiga.
Dk Mahiga alikuwa miongoni mwa makada wa CCM aliyetangaza kuwania nafasi ya urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Akimtangaza jana  Rais Magufuli alimteua pia kuwa mbunge, huku akimtaja Dk Suzan Alphonce ambaye ni mbunge wa Viti Maalumu kuwa naibu wa wizara hiyo mpya.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, naibu waziri aliyeteuliwa kusimamia ni Angelina Mabula ambaye ni mbunge wa Ilemela, Mwanza.
 Katika Wizara ya Maliasili na Utalii ambayo haijapata waziri, Rais Magufuli amemteua Mhandisi Ramon Makani kuwa naibu waziri wa.
Sura nyingine mpya ni ya Mhandisi Stella Manyanya ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
 Dk Khamisi Kigwangalla ambaye alikuwa mmoja wa makada wa CCM waliotangaza nia ya kuwania nafasi ya urais, ametuliwa kuwa naibu waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto huku Mhandisi Isack Kamwela (mbunge wa Katavi) akiteuliwa kuwa naibu waziri Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

No comments :

Post a Comment