Msemaji wa wamiliki wa kituo hicho wamewaahidi wananchi kuwa kituo kinasukumwa nyuma na huduma wananchi wataendelea kupata kama kawaida kuanzia January Mosi, 2016.
"Katu wateja wetu hawatopata shida. Hatua za haraka tunazichukuwa na huduma itaanza as early as 1st January, 2016, kama muandishi unavyojionea mwenyewe. Tunafanya kazi usiku na mchana", alieleza msemaji wa wamiliki wa kituo hicho ambae alijitambulisha kwa jina la Ngida pale alipohojiwa na blog hili la Zanzibar Ni Kwetu.
"Ndugu muandishi, sisi hapa ni kazi tu, malalamiko baadae. Barabara ikipanuliwa italeta manufaa kwa wengi. In fact, gari nyingi zitatoka mjini kuja kutia mafuta hapa kituoni kwetu kama barabara ni safi. Kwahivyo, hichi ni kitendo cha maendeleo kinachotekelezwa na SMZ na tunakiunga mkono mia kwa mia. Barabara safi ni jambo moja zuri nchi yetu inataka", alimalizia msemaji huyo wa Fuoni Petrol Station.
Kituo cha mafuta cha Fuoni kikibomolewa kwaajili ya utanuzi wa barabara ya Fuoni, Zanzibar.
Jengo la gorofa mbili linalotakiwa kubomolewa sehemu ya mbele ya jengo hilo baada ya kuwekwa alama kuvunja ili kupisha utanuzi wa barabara hiyo ya fuoni, likiwa tayari mmiliki wa jengo hilo tayari ameshaaza kubomoa sehemu ya mbele ya jengo hilo kwa kutoa madirisha na mageti.
Alama inayotakiwa kuvunjwa ili kupisha utanuzi wa barabara hiyo ikiwa imewekwa alama ya kuvunjwa sehemu hiyo.
Sehemu ya barabara hiyo tayari imeshatiwa kifusi.
Hali ya maadhari ya eneo hilo la ujenzi wa barabara mpya likiwa safi baada ya kukatwa kwa miti na nyumba zilizojengwa kando ya barabara hiyo.
Wananchi wakiangali zoezi la kuondoa visiki vya miembe baada ya miti hiyo kukatwa ili kupisha zoezi hilo.
Hali ya usafi na kuaza kuweka kifusi katika ujenzi wa barabara hiyo tayari umeshaaza. |
Burdoza likingowa kiziki cha muembe eneo la fuoni ili kupisha utanuzi wa barabara hiyo.
No comments :
Post a Comment