Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, December 14, 2015

Waziri Nchemba aingilia kati mapigano ya wakulima, wafugaji Mvomero



Morogoro. Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba ameiagiza kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Mvomero kuimarisha ulinzi maeneo yote yenye migogoro kufuatia kutokea  mapigano kati ya wakulima na wafugaji na kuua mtu mmoja na kujeruhi wengine kadhaa.
Waziri Nchemba ametoa agizo hilo leo baada ya kutembelea eneo ambapo yalizuka mapigano hayo Jumamosi Desemba 12/2015 katika  kijiji cha Dihinda kata ya Kanga wilayani Mvomero.
Pia Nchemba ameagiza vyombo vya usalama kuhakikisha waliosababisha maafa hayo wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sharia
"Natoa rai kwa Wananchi hususani wa jamii ya Wafugaji na Wakulima, Hakuna ardhi au Mnyama mwenye thamani sawa na Maisha ya Mwanadamu yeyote yule,njia bora na salama ya kutatua migogoro hii inayohusisha wakuliama na wafugaji ni kufuata taratibu za kuonana na Uongozi wa serikali wa eneo husika hatua kwa hatua, ilisema taarifa ya Nchemba nakuongeza kuwa
‘’Nawaomba wananchi waache kujichukulia sheria mikononi, Tunakwenda kuunda kamati za usuluhishi wa migogoro hii kwa kila kijiji zitakazohusisha pande zote mbili ili kubaini wavamizi wa maeneo na kuwachukulia hatua za kisheria."
Imesema taarifa ya Waziri Mwigulu
Licha ya mapigano hayo kuua mtu mmoja na kujeruhi wengine, pia  yamesababisha hasara kubwa ambapo ng’ombe 79 wameuawa kwa kukatwa mapanga na wengine 72 wamejeruhiwa.

No comments :

Post a Comment