dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, December 15, 2015

Hii jamani ni kali sana!!!................'WEWE NI KIBAKA TU............."


Kubenea kizimbani kwa kutoa lugha chafu



Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (mwenye fulana ya mistari) akimsikiliza mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea (wa kwanza kulia) wakati walipokuwa kiwanda cha nguo cha Tanzania Tooku kujaribu kutatua mgogoro wa wafanyakazi kabla ya kutofautiana na Makonda kuamuru mbunge huyo kukamatwa na polisi jana. Picha na Venance Nestory
By Tausi Ally, Nuzulack Dausen na Peter Elias, Mwananchi
Dar es Salaam. Mbunge wa jimbo Ubungo kupitia Chadema, Saed Kubenea amepandishwa kizimbani kortini Kisutu, jijini Dar es Salaam leo na kusomewa shtaka la kutoa lugha chafu dhidi ya Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.
Hata hivyo, Kubenea amekana kufanya kitendo hicho na kesi yake kuahirishwa hadi Desema 29, mwaka huu huku uchunguzi ukiendelea.
Taarifa iliyotolewa na gazeti la Mwananchi kuhusu Kukamatwa kwake jana
Mbunge wa Ubungo (Chadema), Said Kubenea amekamatwa na polisi kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salam, Paul Makonda baada ya kudaiwa kurushiana maneno wakati wakitatua mgogoro wa wafanyakazi wa Kiwanda cha ushonaji na usafirishaji wa nguo, Tooku.
Viongozi hao walitofautiana kauli baada ya Makonda kudaiwa kumkatalia Kubenea kuzungumza na wafanyakazi hao.
Akizungumza na gazeti hili akiwa Kituo cha Polisi Magomeni ambako alikuwa akishikiliwa, Kubenea alisema alikuwa wa kwanza kufika kiwandani hapo na kuzungumza na wafanyakzi hao na baadaye uongozi na wakati wako katika majadiliano, Makonda aliingia.
“Nilimwelezea tulipofikia na baadaye akasema anataka kuzungumza na wafanyakazi,  lakini alitaka kumaliza mkutano bila kunipa nafasi. Nilimuuliza, mbona hunipi nafasi, akasema mimi ni nani, yeye ndiyo mkuu wa wilaya, tukabishana na mimi nikamwambia ‘wewe ni kibaka tu,” alidai Kubenea.
kizungumzia suala hilo, Makonda alidai kuwa mbunge huyo alionekana kutofahamu taratibu za kutatua migogoro na nguvu aliyonayo mkuu wa wilaya kutokana na ugeni wa kazi ya ubunge.A
Makonda alisema alipofika alifanya kikao cha ndani na uongozi wa kiwanda na kuhudhuriwa na Kubenea ambaye baadaye alizungumza na wafanyakazi hao.
“Lakini wakati nawasikiliza wafanyakazi, Kubenea alitaka naye kuongea, ile haikuwa nafasi yake kwa kuwa alishawasikiliza, lakini aling’ang’ania kutaka kuzungumza,” alidai Makonda.
Alidai baada ya Kubenea kuona hajapatiwa nafasi ya kuzungumza, alianza kumrushia matusi jambo ambalo halikumfurahisha, hivyo kuamuru polisi kumkamata na kumhoji kwa matusi hayo.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Camilius Wambura alipoulizwa kuhusiana na suala hilo, alisema walikuwa wanaendelea kumhoji mbunge huyo pamoja na watu wengine. Hii ni mara ya pili kwa Makonda kuamuru kuswekwa rumande kwa viongozi baada ya baadhi ya  maofisa  wa ardhi wa Manispaa ya Kinondoni kuchelewa kufika kwenye  utatuzi wa mgogoro wa ardhi  Kata ya Wazo.

No comments :

Post a Comment