Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, January 22, 2016

Asha Bakari Makame kuzikwa leo

Asha Bakari Makame
Mwili wa Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Asha Bakari Makame, aliyefariki dunia Dubai akitokea India kwenye matibabu, anatarajiwa kuzikwa leo Kianga, mkoa wa Mjini Magharibi.
 
Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya mwili wa marehemu kuwasili jana na Shirika la Ndege la Qatar, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud Mohamed, alisema ibada ya kumwombea dua itafanyika katika Msikiti wa Mombasa kwa Mchina,  saa 3:30 asubuhi.
 
Alisema Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, anatarajia kuongoza maziko hayo. Pia viongozi wa kitaifa wanatarajia kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wakiwemo wa chama na serikali.
 
Alisema marehemu Asha atakubukwa kwa mchango wake mkubwa katika utumishi wa serikali na CCM kwa nyadhifa mbalimbali alizoshika wakati wa uhai wake.Alisema Asha alikuwa kiongozi jasiri, muwazi na mkweli katika kutetea misingi ya Mapinduzi na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
 
Upande wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema chama kimepata pigo kubwa kwa kuondokewa na kiongozi wake makini na mchapakazi katika siasa za Muungano na Zanzibar.
 
Mwanasiasa huyo alizaliwa Desemba 25, 1949 huko Mtambwe, Pemba na kupata elimu ya msingi katika shule ya Utaani kuanzia mwaka 1957 kabla ya kujiunga na masomo ya sekondari katika shule ya Fidel Castro mwaka 1965 hadi 1968.
 
Alijiunga na Chuo cha Uhazili mwaka 1969 hadi mwaka 1974 na kuhitimu masomo ya ukatibu muhtasi na mwaka 1979 alipata sitashahada katika taaluma hiyo.
 
Mwaka 1985 alipata diploma ya siasa ya sayansi na utawala na kufanya kazi ya Katibu muhtasi Ofisi ya Rais Pemba, Wizara ya Elimu, Wizara ya Mawasiliano na Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
 
Nyadhifa zyingine alizowahi kushika pamoja na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi mwaka 1988 hadi 1990, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii Vijana na Ustawi wa Wanawake.
 
Pia aliwahi kuwa Waziri wa Ustawi wa Jamii, Wanawake na Watoto, Mjumbe Baraza la Wawakilishi Zanzibar (BLW) Mjumbe wa Halimashauri Kuu pamoja na Katibu wa CCM Wilaya ya Wete na Kaskazini A Unguja.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment