Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, January 14, 2016

Magufuli ampa zawadi ya kiwanja Samatta.


Serikali
ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli, imetoa zawadi ya kiwanja kwa Mbwana Samatta kutokana na mshambuliaji huyo wa TP Mazembe na Taifa Stars kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, jana alimkabidhi Samatta hati ya kiwanja hicho kilicho Kigamboni jijini Dar es Salaam.

“Hii ndiyo hati yenyewe. Ila ukiwa tayari karibu ofisini kwangu ili nikukabidhi hati na vijana wakakuonyeshe kiwanja. Kitakuwa ni kiwanja katika sehemu nzuri kabisa, si zile sehemu watu wamefanya eneo liwe skwata,” alisema Lukuvi.

Mbali na kiwanja, Lukuvi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla ya kumuaga Samatta kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, alitoa zawadi ya fedha taslimu kwa straika huyo matata ambazo hata hivyo, hazikuelezwa ni kiasi gani.“Nimekupa hizi, huu mzigo ni wako kwa niaba ya serikali. Wewe mwenyewe ukiamua kuzionyesha, basi fanya hivyo,” alisema.

Baadaye Samatta alimkabidhi jezi yake TP Mazembe Lukuvi ambaye alisema ataiwasilisha kwa Waziri Mkuu ambaye alimuwakilisha katika hafla hiyo.

Baadaye Samatta pia alitoa jezi kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, ambaye amekuwa karibu yake kwa kipindi kirefu kabla hajaenda Nigeria alikoshinda tuzo ya Mwanasoka Bora na baada ya kurejea.

Nyota huyo wa zamani wa African Lyon na Simba, ametwaa tuzo ya Mwasoka Bora wa Afrika Anayecheza barani baada ya kuiwezesha TP Mazembe kutwaa taji la tano la Klabu Bingwa Afrika mwaka jana huku akiibuka Mfungaji Bora wa michuano hiyo.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment