Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, January 26, 2016

Magufuli atumbua jipu vitambulisho vya taifa

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue
Rais Dk. John Magufuli ameendelea kutumbua majipu, baada ya jana kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu, kwa kile alichokieleza ni matumizi mabaya ya Sh. bilioni179.6 zilizotolewa kwa taasisi hiyo kwa ajili ya kutengeneza vitambusho vya wananchi.
 
Pia Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Mhandisi Madeni Kipande kabla ya kuthibitishwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi kutokana na utendaji kazi usioridhisha.
 
Mbali na utenguzi huo, pia Rais Magufuli amewasimamisha kazi watumishi wanne wa Nida ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili, ambao ni Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), Joseph Makani, Ofisa Ugavi Mkuu, Rahel Mapande, Mkurugenzi wa Sheria, Sabrina Nyoni na Ofisa Usafirishaji, George Ntalima.
 
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu uamuzi huo uliochukuliwa na Rais Magufuli. Aidha, alisema Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa kuwarejesha nyumbani  mara moja aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Japan, Dk. Batilda Buriani na Balozi wa Tanzania nchini Italia, Dk. James Msekela, baada ya mikataba yao kumalizika.
 
“Hivyo Rais ameziagiza Mamlaka ya Udhibiti na Manunuzi ya Umma (PPRA), Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza na kufanya ukaguzi wa Value for Money  (thamani ya fedha) zilizotolea katika taasisi ya Nida kama inaendana na kazi iliyofanyika baada ya kuthibitisha idadi halisi ya vitambulisho vilivyotolewa,” alisema Balozi Sefue.
 
Aidha, Balozi Sefue alisema Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye serikali ya awamu ya nne, Mahadhi Juma Mahadhi kuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Kuwait na kumrejesha nyumbani Balozi wa Tanzania aliyeko London, Uingereza, Peter Kallaghe kwa ajili ya kuja kufanya kazi Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa hadi atakapopangiwa kazi nyingine.
 
“Kwa maana hiyo nchi zifuatazo hazitakuwa na mabalozi, Uingereza baada ya kurejea kwa Kallaghe nchini, Brussels baada ya Balozi Deodorous Kamala kuchaguliwa kuwa Mbunge, Italia baada ya kumalizika mkataba wa Dk. Msekela, Japan kufuatia kumalizika mkataba wa Dk. Buriani, Brazili kufuatia kustaafu Balozi Francis Malambugi na Malaysia baada ya Dk. Aziz Ponray Mlima kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu,” alisema Sefue.
 
VIONGOZI WAONYWA
Balozi Sefue alisema Ikulu haitasita kuchukua hatua dhidi ya kiongozi yeyote na mtumishi mzembe na asiye muadilifu.
 
 WAKUU WA MIKOA, WILAYA
Alisema wakuu wa mikoa na wilaya wanatakiwa kujenga uwezo wa kushughulikia shida za wananchi kwa ukamilifu na kwa wakati.
 
Alisema kila ofisi ya serikali iwe na utaratibu wa kupokea maoni ya wananchi kuhusu huduma inayotolewa kwenye ofisi hizo na kushughulikia haraka maeneo yote ambayo wataonyesha kutoridhika na huduma.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment