Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, January 26, 2016

Mbowe afunguka utata wa kamati

Kiongozi wa Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.
Kiongozi wa Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, amezungumzia uteuzi wa Kamati za Bunge na kusema ingawa Spika wa Bunge ana mamlaka ya kuzipanga, hakutendea haki upinzani pamoja na wabunge wengine waliobobea kwenye maeneo waliyotaka kupangwa kwa kuhofia kwamba wangeibana serikali.
 
Aidha, Mbowe alisema ofisi yake inaendelea na mazungumzo na Spika wa Bunge, Job Ndugai, na kudai kuwa ingawa kanuni zinaruhusu mbunge kuchagua kamati anayotaka, ofisi ya spika haikuzingatia suala hilo.
 
Mbowe aliyasema hayo jana bungeni wakati akizungumza na waandishi wa habari na kufafanua kuwa bado mvutano unaendelea dhidi ya wajumbe wao ambao wamependekezwa kuwa kwenye Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali ya Mitaa (LAAC).
 
“Sisi tunakanuni zinazotuongoza, lakini Bunge limetumika kukandamiza wapinzani na kutuchagulia wawakilishi wanaowataka wao, bila kuzingatia uzoefu wa mbunge aliokuwa nao,” alisema.Mbowe alisema kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, spika ana mamlaka ya kikanuni kuunda wajumbe wa kamati na kufuata vigezo vinavyotakiwa.
 
Aidha, alisema orodha ya majina ya wajumbe hayajapangwa na spika na kufafanua kuwa ukweli ni kwamba amepangiwa na watendaji wake chini ya kivuli cha spika.
 
Alisema wamependekeza majina yao lakini jambo la kushangaza hayakuwekwa kwenye kamati hizo jambo ambalo bado mazungumzo yanaendelea.
 
Mbowe alisema kumewekwa mkakati wa kuwaondoa wabunge wao ambao wanauzoefu katika masula mbalimbali ya kitaaluma na kuwapanga maeneo ambayo uwezo wao utatumika kwa kiwango kidogo.

CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment