Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema jimbo la Iringa Mjini kimekishutumu chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Iringa Mjini kwamba CCM ni miongoni mwa taasisi ambazo hazilipi kodi ya majengo.
Kauli hiyo ilitolewa jana na mbunge wa jimbo hilo Mchungaji Peter Msigwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mwembetogwa vilivyopo mjini Iringa ambapo mkutano huyo uliandaliwa na chama chake kwa lengo la kuwashukuru wananchi kwa ushindi walioupata katika uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana.
Hata hivyo kwenye uchaguzi huo Msigwa alifanikiwa kutetea kiti chake cha Ubunge huku Chadema ikipata madiwani 14 kati ya kata 18 na kuandika historia mpya kwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuongozwa na chama cha upinzani.
Msigwa alisema yeye na chama chake wanaunga mkono jitihadi za Rais wa awamu ya Tano Dk. John Magufuli ya kukusanya kodi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kwamba kwa muda mrefu wananchi wa kipato cha chini ndio wamekuwa wakibanwa kulipa kodi huku matajiri wakikwepa kodi na kuisababisha serikali hasara kubwa.
“Rais Magufuli anasema yeye anatumbua majipu na mimi nitakuwa mwendawazimu kama sitomuunga mkono katika hili,na penye ukweli tuseme bila kumung’unya maneno, wakwepaji kodi ni wafanyabiashara wakubwa, na kwa hapa Iringa Chama cha Mapinduzi ni mkwepaji kodi namba moja”alisema Msigwa na kuongeza.
“Miongoni mwa maeneo ambayo hayalipwi kodi ni uwanja wa mpira wa miguu wa Samora wanaoumiliki, jengo la Ofisi za CCM Mkoa, jengo la ofisi za wilaya zilizoko eneo la sabasaba, shule ya Sekondari ya wazazi ya Mwembetogwa na vibanda vya biashara vya CCM maarufu (Vibanda vya kiti moto, kama wao wanakwepa kodi wanapata wapi uhalila wa kukusanya kodi? alihoji msigwa.
Msigwa alisema chadema kinamuunga mkono Dk Magufuli na wanataka aendelee na kazi ya kutumbua majipu, kwa bahati nzuri mengi yako CCM,wakati akifanya chadema kitamsaidia kukamua na kumuonesha majipu mengine yalipo.
Aidha madai hayo yamepingwa na Kaimu Katibu wa CCM mkoa wa Iringa Elisha Mwampashi ambaye alisema kuwa si kweli kuwa wao wanakwepa kodi kama anavyodai.
Mwampashi ambaye pia ni Katibu wa CCM Manispaa ya Iringa alisema kila mwaka wanalipa kodi kulingana na eneo ambalo jengo lao lipo kwa kuwa wana majengo maeneo mengi na yamekuwa yakilipiwa kodi kulingana na viwango vya maeneo hayo.
Alipotakiwa kutoa ufafanuzi zaidi, alisema ataandaa taarifa na kukutana na wanahabari ili kutoa ufafanuzi juu ya jambo hilo akiwa na vielelezo vinavyoonesha malipo hayo.
“ Msigwa si mkweli katika hili kwa kuwa amekuwa katika nafasi ya Ubunge kwa miaka mitano, anataarifa za Manispaa ya Iringa juu ya mapato yatokanayo na kodi ya majengo yakiwamo majengo yetu”alisema Mwampashi.
Katika hatua nyingine Msigwa aliwataka watu wenye mashamba makubwa ndani ya Manispaa ya Iringa kuanza taratibu za kupima viwanja vyao wenyewe na kuviuza kwa wananchi ama kuiachia Manispaa ivichukue na kuwapimia wananchi kwakuwa sheria ya Mipango miji hairuhusu mtu kuwa na shamba ndani ya miji.
Alisema wapo matajiri wanaomiliki ekari nyingi kwa ajili ya mashamba na kuongeza kuwa sheria ya mipango miji hairuhusu mtu kumiliki eneo kwa ajili ya shamba mjini na kwamba vikao vya baraza la madiwani linaloongozwa na chama vitakapoanza vitashughulikia masuala hayo.
Pia alisema sheria inaruhusu shamba lisilozidi ekari tatu kwa maeneo ya mijini lakini kuna matajiri na wawekezaji hapa mjini wanazaidi ya ekari tatu jambo ambalo ni kinyume na sheria hiyo.
Awali akizungumza kwenye mkutano huo Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe alisema Manispaa hiyo imejipanga kukusanya kodi na kuongeza mapato kutoka Sh 2.4 bilioni zilizokuwa zikikusanywa katika awamu iliyopita hadi kufikia 7 bilioni.
“chadema kimeingia na tumeanza kazi,lengo letu ni kuujenga mji wa Iringa kufikia hadhi ya jiji na ili tuweze kufanikisha hayo kunagharama zinahitajika,tunachowaomba ni kwamba tutahakikisha tunakusanya kodi hususani ya majengo kwa watu wote’alisema Kimbe na kuongeza:
“Tunaanzia pale walipoishia kama wenzetu walikwenda kwa kasi ya kilometa 40 kwa saa sisi tutakwenda 120, tunataka kupanga mji, tuna hospitali tunataka ziwe na madawa, tunataka tuwe na gari la kubebea wagonjwa katika hosptali yetu ya Manispaa …tutakusanya kodi kwa watu wote hususani matajiri ambao ndio wamekuwa wakwepaji wakubwa wa kodi’alisema.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments :
Post a Comment