Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, January 16, 2016

Serikali yaokoa bn3/- madini.

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam.
Serikali imeokoa zaidi ya Sh. bilioni 3 kwa kudhibiti utoroshaji wa madini ambayo yalikuwa yanasafirishwa nje ya nchi kinyume cha utaratibu.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa madini, Tanzania (TMAA), Dominic Rwekaza, kwa vyombo vya habari, katika kipindi cha Julai mwaka jana mpaka Januari 13, mwaka huu kulikuwa na matukio 14 ya utoroshaji wa madini.
 
Ilisema katika matukio hayo, madini yenye thamani ya Dola za Marekani 1,474,194 (sawa na zaidi Sh. bilioni 3.2) yalikamatwa na wakaguzi wa Wakala kupitia madawati ya ukaguzi yaliyopo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Dar es Salaam, Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) na Mwanza. 
 
Taarifa hiyo ilieleza kuwa katika matukio ya hivi karibuni ya ukamataji wa madini katika viwanja vya ndege, TMAA ilikamata madini yenye thamani ya Sh. milioni 11.2 kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola.“Raia mmoja wa kigeni na mwingine wa Tanzania walikamatwa wakiwa na madini hayo bila kuwa na kibali chochote cha usafirishaji kulingana na Sheria ya Madini ya mwaka 2010,” ilieleza taarifa hiyo.
 
Taarifa hiyo ilisema raia huyo wa kigeni ambaye jina lake limehifadhiwa, alikuwa anasafiri kwenda Bangkok, Thailand na alikamatwa akiwa na madini aina mbalimbali ikiwemo almasi, aquamarine, sapphire, green tourmaline, quartz na rhodolite.
 
Katika tukio la pili, raia mmoja aliyekuwa akisafiri kwenda Ujerumani, alikamatwa akiwa na amethyst, moonstone cabochon, rulilated quartz (cabochon), rulilated quartz (faceted), chrysoprase, green tourmaline, ruby, red garnet, green quartz, zircon na rhodolite, ilisema. 
 
TMAA ilisema kuwa watuhumiwa wote waliohusika katika matukio hayo wamechukuliwa hatua za kisheria, ikiwamo kufunguliwa kesi mahakamani.
 
Aidha, Wakala ulitoa rai kwa umma kujiepusha na shughuli za utoroshaji na biashara haramu ya madini, kwani hatua kali zitaendelea kuchukuliwa kwa yeyote atakayebainika kujishughulisha na biashara hiyo kinyume cha sheria.
 
Wakala ulisema madini yatakayobainika kusafirishwa bila kufuata taratibu zilizopo yatataifishwa na serikali.
 
Aidha, serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini ilitoa wito kwa yeyote atakayetoa taarifa za biashara haramu ya madini kwa Kamishna wa Madini au Wakala ambazo zitawezesha ukamataji wa madini, atazawadiwa asilimia tano ya fedha zilizookolewa.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment